Header Ads

Picha: Rais Paul Kagame Atua jijini Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard K. Membe (Mb)
akisalimiana na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame alipowasili katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Kagame yupo nchini kwa
ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Ukanda wa Kati kuhusu Uwekezaji na Viwanda unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Aidha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda walitembelea bandari ya Dar es salaam leo Machi 26, 2015.

Pia, Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wageni wake Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Pierre Nkurunzinza walihudhulia kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015.

Picha chini

No comments

Powered by Blogger.