Header Ads

FALCAO AMTUMIA SALAAM VAN GAAL, APIGA MABAO MAWILI NDANI YA DAKIKA NNE


HUU NDIO UJUMBE: unaweza
kusema hivyo baada ya mshambuliaji wa Manchester United, Radamel Falcao
kumpelekea ujumbe kocha
wake Louis van Gaal kwa
vitendo.

Falcao ambaye amekuwa
akiwekwa benchi katika kikosi
cha Man United, ametupia
mabao mawili ndani ya dakika
nne wakati timu yake ya taifa
ya Colombia ikiivaa Bahrain
katika mechi ya kirafiki.

Aidha, Colombia iliyokuwa ugenini
katika mechi hiyo ya kalenda
ya Fifa, ilishinda kwa mabao
6-0 huku Falcao akifunga bao
la tatu na la nne ndani ya
dakika nne.

Licha ya kuwa kwao, Bahrain
iliyo namba 103 kwa ubora wa
Fifa, ilishindwa kufurukuta
dhidi ya Colombia
iliyoonekana kuwazidi kila kitu.
Kwa mabao hayo mawili,
amefikisha mabao 55 na sasa
Falcao ameshika nafasi ya pili
kwa wachezaji waliofunga
mabao mengi zaidi wakiwa na
kikosi cha timu ya taifa ya
Colombia.

WAFUNGAJI BORA COLOMBIA:
1. Arnoldo Iguaran 24 mabao, mechi 68

2. Radamel Falcao mabao 23, mechi 55

3. Faustino Asprilla mabao 20, mechi 57

4. Freddy Rincon mabao 17, mechi 84

5. Víctor Aristizabal mabao 15, mechi 66

6. Teofilo Gutierrez mabao 14
mechi 37

7. Adolfo Valencia mabao 14
mechi 37

8. Ivan Valenciano mabao 13
mechi 29

9. Antony de Avila mabao 13
mechi 54

10. James Rodriguez mabao, 12 mechi 32

11. Willington Jose Ortiz mabao, 12 mechi 49

No comments

Powered by Blogger.