Header Ads

Rais Kikwete Ateua Wabunge Wawili Wapya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua
wabunge wawili (2) wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais amefanya uteuzi huu kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e) ambapo amepewa mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi 10.

Walioteuliwa ni Dkt. Grace Khwaya Puja na Bwana Innocent Sebba.

Uteuzi huu umekamilisha idadi ya wabunge ambao Mheshimiwa Rais amepewa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Kikatiba.

Wabunge ambao wameshateuliwa ni:
- Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
- Mhe. Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo
- Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro
- Mhe. Janet Zebedayo Mbene
- Mhe. Saada Salum Mkuya
- Mhe. Zakhia Hamdani Meghji
- Mhe. Shamsi Vuai Nahodha
- Mhe. James Fransis Mbatia

Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Machi, 2015.

No comments

Powered by Blogger.