Header Ads

Moto wawaacha wanafunzi 400 bila makao UDSM

Wanafunzi wapatao 400 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambao wanaishi katika mabweni ya Mabibo hawana mahali pa kuishi
baada ya moto kuharibu sehemu ya bweni hilo jana.

Uongozi wa chuo kikuu uliwaomba wanafunzi kuondoka kwenye block B na A ya bweni hilo ili kupisha uchunguzi.

Wanafunzi wawili walijeruhiwa wakati wa tukio hilo, akiwemo msichana ambaye aliruka
kutoka gorofa ya pili kuokoa maisha yake. Walipekelekwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Moto, ambao chanzo chake hakikuweza kujulikana kwa haraka, ulichoma stoo ya magodoro yaliyokuwa yamehifadhiwa na
kusambaa katika vyumba vingine vitano ambavyo viliharibiwa kabisa.

Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Rwekaza Mukandala, alisema uchunguzi umeonyesha kwamba jingo lililoungua haliko salama kwa
makazi baada ya kupata ufa mkubwa. Na hivyo kuwaomba wanafunzi watoke humo.

“Tumewaagiza wanafunzi wote wa upande huu kuondoka na kupewa sehemu nyingine kwa ajili ya makazi huku jengo hilo likikarabatiwa,” alisema Profesa Mukandala.

Chanzo: The Citizen

No comments

Powered by Blogger.