FID Q KUACHIA WIMBO NA SAUT SOL -KENYA
Akiongea jana kwenye kipindi cha Mambo Mseto cha Citizen Radio ya Kenya, Fid amedai kuwa
wimbo huo wameurekodi juzi usiku.
“Nilikuja Nairobi kwaajili ya kurekodi na Sauti Sol, namshukuru Mungu tumefanya session last night
na kiukweli wote tumeondoka happy,” Fid alimwambia mtangazaji wa kipindi hicho, Mzazi
Willy Tuva.
“Naposema hivyo namaanisha kuwa tumefanya ngoma fulani hivi ambayo wengi hatukuitajia kama ingekuwa nzuri hivyo, Ninachoshukuru ni ile chemistry ndani ya studio, Studio tulikuwa wengi kidogo kwahiyo tumejaribu kushare ideas kidogo, watu wasubiri kitu fulani ambacho kitakuwa amazing kidogo,” aliongeza.
Hata hivyo, Katika hatua nyingine Fid alisema amepunguza
spidi ya kuachia ngoma mara kwa mara kwakuwa amegundua nyimbo zake zinahitaji muda mrefu
kueleweka kwa mashabiki wake.
Aidha, Alisema kuwa amegundua kuwa nyimbo zake hazishuki chart na kwamba hata wimbo mmoja tu
kwa mwaka unatosha.
Pia, Alizungumzia tatizo la wasanii wengi wa hip hop kushindwa kufanya vizuri na kusema kuwa
wengi wanaimbiana wao kwa wao na sio kutoa nyimbo zinazogusa maisha ama hisia za
mashabiki.
“Unakuta mtu anapiga labda ‘mimi sijui napita na metaphors kadhaa, sijui utaniambia nini’ sasa hiyo
wale akina mama ambao wako uswahili kule hawaelewi tunaongea kuhusu nini,” alisema.
“Mara nyingi tunaimba ‘mimi ni mkali kuliko wewe, mimi ni noma, mimi ni nini’, kwahiyo inakuwa
kama unawaambia wasanii wenzako, hauwaimbii wananchi, Inaeleweka kuwa ni mistari ya hivyo
lakini sio album nzima,” alisisitiza.
“Kwahiyo unakuwa kama emcee wa battle, Unakuta mtu anaweza akashinda kwenye battle field lakini hawezi kutoa hit song, tukumbuke kwamba muziki upo kwaajili ya kuwaambia wananchi, kuwaambia watu, kwahiyo tuwaimbie watu, tuongee nao kuhusiana na vitu vinavyowahusu wao, Muziki kwa namna fulani lazima ureflect community kwa ujumla.”
Source; BONGO5
Post a Comment