Header Ads

TAARIFA KAMILI YA WALIOFARIKI KWA MVUA HUKO - KAHAMA

Watu 38 wamefariki dunia na
wengine 82 wamejeruhiwa baada ya
kuangukiwa na nyumba kutokana na mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo kunyesha usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Mwakata Kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani
Shinyanga.

Akiwa eneo la tukio, Kamanda wa
polisi mkoa wa Shinyanga Justus
Kamugisha amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo, na kusema waliokufa
wengi ni watoto ambao walisombwa
na maji baada ya maji kujaa ndani ya nyumba zao na kwamba majeruhi walelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama.

Aidha, Kamanda Kamugisha amesema watu 35 wamekufa eneo la tukio na wengine watatu wamekufa walipofikishwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama na kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka kutokana na
majeruhi wengine kuwa na hali
mbaya.

Amesema majina ya waliokufa kwa
sasa bado hayajatambulika na
kwamba kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Shinyanga inakaa jioni hii ili kutathimini maafa hayo pamoja na kujua ni msaada gani unahitajika kwa
wahanga hao.

Naye, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya ya Kahama,
ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo
Benson Mpesya amesema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya itakaa kabla ya kamati ya mkoa ili kupata taarifa zitakazoisaidia serikali kuanza kutoa misaada.

Nyumba zimeharibika vibaya,ambapo Mkuu wa mkoa wa
Shinyanga aliyefika eneo la tukio na kusema kuwa nyumba 500 zimeharibiwa na mvua hiyo.

Pia, Mpesya ametoa agizo kwa uongozi Redcross na jeshi la Scauti kuhakikisha wanasaidia katika familia zilizokutwa na maafa
hayo wakati serikali ikisubiri
kukamilika kwa zoezi la sense ya
wahanga hao aliloagiza kufanywa na viongozi wa eneo hilo.

Source; Malunde blog

No comments

Powered by Blogger.