Header Ads

FAHAMU; MWANDISHI WA HABARI BBC ANAYEVAA 'OVYO'


Pichani (hapo chini) ni Raphael Tenthani, huenda akawa mfanyakazi mchafu ambaye anaewakilishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) nchini Malawi.

Aina yake ya mavazi na uvaaji wake umezua gumzo katika mitandao jamii, amezoeleka kuonekana katika
mavazi ya 'hovyo hovyo', yaliyolowa, machakavu na
yaliyotoboka huku viatu vikiwa
vimeachama, nywele 'vululu
vululu' na sura ya 'kilevi'.

Aidha, Mwandishi huyu wa habari hujihudhurisha alivyo katika
kazi zake mbalimbali za kuhojiana na kurusha habari bila kujali ustaarabu wa eneo husika hata ikiwa ni kwenye zulia jekundu.

Hata hivyo, Wengi wanasema mkosoaji huyu mkubwa wa Serikali zote zilizoongozwa na Marais ndugu, Bingu (marehemu) na Peter Mutharika, huendaanafanya hivyo ili kutimiza masharti ya 'mganga'
aliyemsaidia kupata ujasiri,
akili nyingi na kazi katika
shirika kubwa la utangazaji la BBC.

Pia, Wanadai ikiwa atakiuka masharti hayo, huenda akapoteza kazi yake na kuwa 'juha', Vyovyote viwavyo, Raphael "Ralph" Tenthani bado ni mwakilishi wa BBC nchini Malawi.

No comments

Powered by Blogger.