Header Ads

DI MARIA AREJEA KUONGEZA NGUVU KIKOSI CHA MAN UNITED

WINGA Angel di Maria anaweza kurejea kikosini Manchester United wakati wa mechi na Aston Villa baada ya kupona maumivu ya nyama yaliyomuwek nje kwa mechi tatu zilizopita.

Mchezaji huyo aliyesajiliwa United kwa dau la rekodi la Pauni Milioni 59.7, Jana alifanya mazoezi na kikosi cha kwanza na yuko tayari
kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya kocha Louis van Gaal wakati Mholanzi huyo Dutchman anatazamiwa kuendeleza wimbi la ushindi katika mechi saba mfululizo.

Hata hivyo, kocha huyo United hatamharakisha Di Maria kurejea uwanjani na amemuonya kwamba
kama Radamel Falcao, anatakiwa kutulia.

No comments

Powered by Blogger.