Header Ads

ARSENAL YAIZIMA GALATASARAY 4 - 1, YATINGA 16 BORA - MABINGWA ULAYA

KLABU ya Arsenal imefanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Kundi D, Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutinga hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo kufuatia ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji Galatasaray nchini Uturuki.

Lukas Podolski aliifungia The Gunners bao la kwanza dakika ya tatu, kabla ya Aaron Ramsey kufunga la pili dakika ya 11 na la tatu dakika ya 29.

Kiungo mkongwe wa Uholanzi, Wesley Sneijder aliifungia Galatasaray bao la kufutia machozi kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 87, kabla ya Padolski kufunga la nne kwa Arsenal
dakika ya 90.

Mechi nyingine ya kundi hilo, Borussia Dortmund imetoka sare ya 1-1 na Anderlecht ya Ubelgiji.

Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Debuchy/O'Connor dk77, Mertesacker, Chambers, Bellerin, Flamini/Zelalem dk45, Oxlade-Chamberlain, Ramsey/Maitland-Niles dk45, Campbell, Podolski na Sanogo.

Galatasaray: Sinan, Camdal/Alintop dk45, Kaya, Balta, Telles, Melo, Colak, Bruma/Adin dk77, Yilmaz/Oztekin dk45, Sneijder, Bulut na Hamzaoglu.

No comments

Powered by Blogger.