Header Ads

Hosni Mubarak Afutiwa Kesi ya Mauaji - Misri

Mahakama ya Misri imefuta mashtaka yanayomkabili Rais wa zamani Hosni Mubarak dhidi ya mauaji waandamanaji 239 wakati wa machafuko dhidi yake mwaka 2011.

Chumba cha mahakama mjini Cairo
kilishangilia wakati hakimu alipohitimisha kusikiliza na kuamua kufuta kesi hiyo Mashtaka dhidi ya maafisa saba wa juu wa Mubarak, akiwemo waziri wa mambo ya ndani, pia yalifutwa.

Mubarak (86) anatumikia kifungo cha miaka mitatu jela kwa ubadhirifu wa fedha za umma.

Aidha, Mubarak na waziri wake wa mambo ya ndani, Habib al-Adly, na wengine sita walikuwa wameshtakiwa kwa njama za kuua na walihukumiwa kifungo cha maisha gerezani mwezi Juni 2012, lakini kesi iliombwa kusikilizwa tena kiufundi.

Hata hivyo, Zaidi ya watu 800 wanahofiwa kupoteza maisha wakati vikosi vya usalama
walipopambana majuma kadhaa kabla ya Mubarak hajajiuzulu Februari 11, 2011.

Bifya kuona Video dakika 5, Akitoka mahakamani DOWNLOAD

No comments

Powered by Blogger.