MOURINHO: MAKOCHA 'WASIOPAKI BASI' PUMBAVU KABISA, MPIRA USHINDI
KOCHA
wa Chelsea, Jose Mourinho amejibu madongo anayotupiwa na wapinzani wake
juu ya staili yake ya uchezaji wa kujiami na kushambulia kwa
kushitukiza, akisema makocha ambao hawatumii mfumo huo maarufu kama
'kupaki basi' ni wapumbavu.
Mourinho
ameiongoza Chelsea kutwaa taji la Ligi Kuu ya England, lakini mabingwa
hao walibezwa kwamba walikuwa wanakera kwa soka yao ya 'kuoaki basi'.
Kocha
wa Manchester United, Louis van Gaal na wa Arsenal, Arsene Wenger ni
miongoni mwa waliobeza staili ya Chelsea kutomiliki mpira na kushambulia
kwa kushitukiza.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amejibu makocha wanaobeza staili yake ya kupaki basi akiwaita wapumbavu
Lakini
Mourinho amejibu mapigo huku akisema kwamba amepanga kutetea taji hilo
msimu ujao, ingawa ni mezi mwili sasa kabla ya ligi hiyo kuanza tena
Agosti 8.
"Hakuna
kizazi kipya (cha makocha),"amesema Mourinho. "Kilichopo, ni watu kuwa
na mbinu fulani, falsafa fulani, na kutaka kubuni vitu vya aina fulani;
"Tunajipanga vizuri kuanzia nyuma, sisi ni wamiliki wazuri wa mpira,
hatushambulii kwa kushitukiza,".
"Lakini
kama huchezaki kwa mashambulizi ya kushitukiza ni kwa sababu wewe ni
mpumbavu. Mashambulizi ya kushitukiza ni babu kubwa katika soka, ni
silaha ambayo unakuwa nayo, na unapogundua udhaifu wa mpinzani wako,
unakuwa furwa nzuri ya kufunga bao,".
"Hivyo nafikiri watu wanabuni (ujanja ujanja) na umeteka hisia za watu. Lakini soka haiwezi kubadilika. Soka ni ushindi.'
Arsene Wenger alikerwa na uchezaji wa kujihami wa Chelsea Uwanja wa Emirates.
Akizungumza na Sunday Times,
Mourinho pia alithibitisha mpango wa kumtaka mshambuliaji wa Monaco
aliyeshindwa kung'ara akicheza kwa mkopo Manchester United, Radamel
Falcao ili akazibe pengo la Didier Drogba anayeondoka na akasema yuko
kwenye orodha fupi ya wachezaji watano anaowataka.
Mourinho amethibitisha dhamira ya kumtaka Radamel Falcao akazibe pengo la Didier Drogba
Post a Comment