Dkt. Nchimbi Atangaza Kutogombea Songea
Mbunge wa Songea mjini Dkt Emmanuel Nchimbi ametangaza rasmi kutogombea tena ubunge katika jimbo, katika mkutano wa hadhara ambapo baadhi ya wanachama wa CCM wameonesha
kutokubaliana na uamuzi huo.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya wananchi wakiwemo wanachama wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) jimbo la Songea mjini mkoani Ruvuma, wamejikuta katika hali ya sintofahamu
huku wengine wakimwaga machozi baada ya mbunge wa jimbo hilo, mh. Dkt. Emmanuel Nchimbi kutangaza rasmi kutogombea tena ubunge
katika jimbo hilo. Katika uwanja huu wa majimaji mjini songea, mbunge wa jimbo la Songea mjini, mh. Dkt.
Emmanuel Nchimbi aliyelitumikia jimbo hilo kwa miaka 10 akakutana na wanachama wa chama cha mapinduzi pamoja na kuelezea mafanikio mbalimbali ya maendeleo aliyoyafanya katika jimbo hilo ikiwemo ujenzi wa barabara, zahanati na shule za sekondari lakini pia akatumia nafasi hiyo kutangaza rasmi kutogombea tena ubunge katika jimbo la songea mjini.
Tamko hilo la dkt. Nchimbi likazua simanzi kwa baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM hapa Songea huku wengine wakishindwa kujizuia na kujikuta wakimwaga machozi.
Aidha, Katika maelezo yao wanachama hawa wanasema kuachia ngazi kwa Dkt, Nchimbi kutogombea katika jimbo hilo kunatoa fursa kubwa kwa vyama vya upinzani kuchukua jimbo hilo hali ambayo hawakubaliani nayo.
Hata hivyo wanachama hao wakamuomba mbunge huyo kutengua msimamo wake na kumtaka arejee tena kugombea jimbo la Songea mjini, jibu la dkt.
Nchimbi ikawa anaenda kufikiria.
Source; EATV
Post a Comment