ALIYEUA MTOTO AFIKISHWA MAHAKAMANI, APIGWA NGUMI MBELE YA POLISI - MOROGORO
Msichana
Judith Chomile(15) amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa
Morogoro akikabiliwa na tuhuma za kumnyonga hadi kufa mtoto mwenye umri
wa miaka 9 mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Bernard
Benderi ya mjini Morogoro.
Akisoma
shitaka mbele ya hakimu mkazi Ivan Msaki, mwendesha mashataka wa polisi
Aminata Mazengo amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo may 20 kinyume na
kifungu namba 196 cha kanuni ya adhabu nahakutakiwa kujibu lolote
kutokana na kosa lenyewe na kuwa mtuhumiwa yuko chini ya miaka 18 hivyo
kuwakilishwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 10 mwaka huu itakapo tajwa tena mahakamani hapo .
Katika
hali isiyo ya kawaida ndugu wa marehemu Edga Mafwere kwa hasira amempiga
ngumi mtuhumiwa muda mfupi baada ya kutoka mahakamani mbele ya maafisa
wa jeshi la polisi na ustawi wa jamii ambapo naye alijikuta katika
mikono ya jeshi la polisi na kufungwa pingu ambapo anashikiliwa kwa
mahojiano zaidi.
Akizungumza
juu ya uhakika wa usalama wa mschana Judith Chomile ,afisa ustawi wa
jamii manispaa ya Morogoro Jasmin Masenge amesema msichana huyo atakuwa
katika mikono salama chini ya uangalizi wa kitengo cha ustawi wa jamii
pamoja na jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia na watoto hadi
kesi inayomkabili itakapotolewa hukumu.
Post a Comment