Header Ads

PICHA: POLISI ANUSURIKA KUUAWA KWA KIPIGO CHA WANANCHI MOROGORO

Askari mmoja wa jeshi la polisi ambao hutumia pikipiki kufanya doria , aliyejulikana kwa jina la Ramadhani, amenusurika kuuawa jana mchana na wananchi wenye hasira mjini Morogoro kwa kutuhumiwa kusababisha ajali ya dereva wa bodaboda ambaye aliparamia lori .

Tukio hilo linawahusisha askari wawili wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU ) waliokuwa wakiendesha pikipiki yenye namba za usajili za PT 823 ambayo ni mali ya polisi .

Mashuhuda wamesema kwamba polisi haowalikuwa wakimfukuza dereva huyo wa bodaboda ambaye alikwenda kujikita katika lori ambapo wananchi waliwatuhumu kusababisha ajali hiyo na kuanza kuwashambulia.

Baada ya kuona hivyo , polisi hao walianza kurusha risasi hewani lakini wananchi waliwakabili kwa
kuwarushia mawe na hivyo kumjeruhi polisi mmoja.

No comments

Powered by Blogger.