Header Ads

NYALANDU: TEMBO KUTOWEKA MIAKA 10 IJAYO TANZANIA

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro
Nyalandu amesema kama watanzania wasiposhirikiana katika kudhibiti ujangili wa Tembo waliopo watatoweka kabisa katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

Kauli hiyo ameitoa jana kwenye mkutano wa ushirikishwaji wa jamii katika masuala ya uhifadhi wa wanyamapori uliofanyika wizarani kwake.

“Uhifadhi kama tunavyoujua, hautaweza kufanikiwa kama kila mtu kwenye nchi hii atafikiria ni kazi ya serikali kuu peke yake. Na vilevile kama kila mtu atafikiria ni kazi ya wahifadhi peke yao”. alisema Nyalandu kwenye mkutano huo.

Nyalandu alibainisha kuwa, majadiliano hayo, yatakuwa chachu kubwa ya maendeleo katika wizara hiyo huku akiwashukuru wadau hao mbalimbali wakiwemo wanahabari kwa kufika kwao, ili kuangalia suala la uhifadhi kwa mapana yake.

Alisema wakati ujangili wa Tembo nchini umeshamiri sana, wakati umefika kwa watanzania kuhakikisha kwamba wanakomesha hali hiyo ili taifa kuendelea kuwa na wanyama wake.

Kwa upande wake, Ali Said Mosee
aliyehudhuria mkutano huo kutoka
Tanzania Association on Climate Change, alishauri ushirikishaji wa wadau mbalimbali kutatua migogoro kwenye mipaka ya mbuga na pia mgongano wa kimaslahi kati ya hifadhi na wanadamu.

Hata hivyo, Alisema mathalani Tembo katika hifadhi ya Selous wamepungua kutoka Tembo 38,975 katika sensa ya mwaka 2009 hadi Tembo 1,384 kwa sensa ya mwaka 2014 na akasema kwa kasi hiyo katika miaka 10 ijayo Tembo
Tanzania wataisha kabisa.

No comments

Powered by Blogger.