Header Ads

KUTANA NA NYUMBA ZA MAAJABU DUNIANI HAPA



 
Basi mtu wako nikakutana na bonge la HEADLINE mtandaoni yani.. “10 of the Coolest Homes in the World“, nikaingia faster nijionee PICHAZ ya hizo nyumba kali huko DUNIANI.
Nilizokutana nazo kiukweli ilibidi nicheke,alafu nikaona sio vibaya na wewe mtu wanguvu uzione labda iko itakayokuvutia na wewe ukatamani siku moja uwe nayo.

Unaambiwa hii inaitwa Antilia, iko India. Nayo iko kwenye list mtu wangu.

Inaitwa Bio Climatic Solar House, iko Ufaransa. Ilivyokaa kaa ni kama sio mjengo wa kuishi yani.

Boeing 727 House, hii sio mara ya kwanza kuiona mtu wangu. Haikunishtua nilipoiona tena.

Ilinipa tabu kujua nini kinaendelea hapa. Naona kama mapango mapango tu hivi, lakini nd’o mjengo huo yani. Bubble House, iko Ufaransa.

Duuh, jina lake tu ni balaa yani. Inaitwa Crazy House, iko Vietnam.

Mjengo huu uko Ivory Coast, hivi kama kuna watu mjusi tu wanaogopa, itakuwa kulala kwenye huyu mamba? Nyumba hiyo, inaitwa Crocodile House.

Hii nayo ni ghorofa ya aina yake yani. Dar-al-Hajar, iko Yemen huko.

Buti la kijeshi??? Hapana, huo ni mjengo kabisa mtu kajitengenezea hapo, inaitwa Shoe House, iko South Africa.

Hii ya Korea Kusini nayo iko kwenye list, inaitwa Toilet House, kwa juu ukiicheki ni kama choo kweli.

Hiyo Toilet House ya Korea inavyoonekana kwa juu.

Kama imepinduka hivi.. kumbe hapo nd’o iko sawa. Hujaipenda hii mtu wangu? Wenyewe wanaiita The Upside Down House, iko Poland.
Nitafurahi kuona umendikia nyumba ipi imekuvutia zaidi kati ya hizo mtu wangu !!

No comments

Powered by Blogger.