SHEIKH PONDA AIGEUKIA MAHAKAMA, AIOMBA ITUMIE BUSARA KUSIMAMISHA KESI YA UCHOCHEZI INAYOMKABILI
KATIBU
wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda,
ameiangukia Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kwa kuiomba itumie
busara kusimamisha kesi ya uchochezi inayomkabili mkoani Morogoro.
Maombi hayo yaliyokwama mara kadhaa kutokana na sababu za kisheria, yaliwasilishwa jana kupitia wakili wake, Juma Nassoro, wakati rufaa yake ya kupinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyomtia hatiani kwa kuingia kwa jinai katika kiwanja cha Chang’ombe Markaz na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nje, ikisikilizwa.
Maombi hayo yaliyokwama mara kadhaa kutokana na sababu za kisheria, yaliwasilishwa jana kupitia wakili wake, Juma Nassoro, wakati rufaa yake ya kupinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyomtia hatiani kwa kuingia kwa jinai katika kiwanja cha Chang’ombe Markaz na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nje, ikisikilizwa.

Wakili
Nassoro akiwasilisha maombi hayo mbele ya Jaji Augustine Shangwa,
aliiomba mahakama hiyo isimamishe kesi ya uchochezi inayomkabili Ponda
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, hadi itakapotoa uamuzi wa
rufaa hiyo.
“Mheshimiwa
jaji endapo Mahakama ya Morogoro ikimtia hatiani Ponda na kumhukumu
wakati Mahakama Kuu ikikubali hoja zake za rufaa na kutengua hukumu ya
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, itaishushia hadhi mahakama.
“Mahakama
ikisimamisha kesi ya Morogoro, upande wa Jamhuri hautaathirika kwa
kuwa ndio waliofungua kesi, naomba mahakama yako tukufu itumie busara
kusimamisha kesi hiyo,” alidai Nassoro.
Katika rufaa hiyo, Ponda anadai hakukuwa na ushahidi wa kutosha kumtia hatiani kwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.
Ponda
na wenzake walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama, wizi wa
mali yenye thamani ya Sh milioni 59.6 na kuingia kijinai kwa nia ya
kujimilikisha isivyo halali eneo la ardhi inayomilikiwa na Kampuni ya
Agritanza Ltd na uchochezi.
Katika
hukumu iliyotolewa Mei 9, 2013, Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa wa
Mahakama ya Kisutu alimtia hatiani Ponda peke yake kwa kosa la kuingia
kijinai katika eneo la Agritanza Ltd, na ikawaachia huru washtakiwa
wengine wote.
Jaji Shangwa aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 10, mwaka huu kwa ajili ya upande wa Jamhuri kujibu hoja za Sheikh Ponda.


Post a Comment