Header Ads

Baba yake Floyd Mayweather amtaka mwanae ampige 50 Cent ulingoni






Madongo ya 50 Cent kwa bondia Mayweather kuhusu uwezo wake wa kusoma yamemgusa baba yake Floyd Mayweather ambaye amemwambia mwanae dawa ya kukomesha kelele hizo ni kumpa
kichapo heavy tena jukwaani.

Kwa mujibu wa TMZ, baba yake Mayweather ameeleza hayo wakati akifanya mahojiano na Brian Shapiro wa ‘Fox Sports 670’ na kueleza sababu za kumshauri hivyo mwanae.

“50 Cent anaonekana kama ana matatizo tangu Floyd alipomuacha. Ni mwimbaji maarufu duniani lakini anafanya vitendo vya kitoto.” Amesema mzee huyo.
“Muache apambane na Floyd…halafu tukio hilo liwekwe kwenye video. Floyd atayamaliza yote hayo. Hakutakuwa na mengine yakusemwa.” Ameongeza.

No comments

Powered by Blogger.