Robin van Parsie Avishambulia Vyombo Vya Habari Kwa Uzushi
Mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi na klabu ya Man Utd,
Robin Van Persie ameshangazwa na taarifa za kukaribia kufanyiwa upasuaji
katika
goti la mguu wake wa kushoto, taarifa ambazo ameziita ni za kipuuzi.
van Persie amesema suala la yeye kwenda kufanyiwa upasuaji halina ukweli wowote zaidi ya vyombo vya habari kuanza kutengeneza mazingira ambayo yataonyesha huenda kusajiliwa kwa Radamel Falcao kulitokana na janga hilo.
Amesema kusajiliwa kwa Falcao ni mipango ya meneja Louis Van Gaal kwa ajili ya kuboresha kikosi cha Man Utd, na wala si kwa ajili ya kuhitaji kufanyia upasuaji.
Aidha van Persie amesema amezungumza na Falcao na kumkaribisha katika kikosi hicho huku akisisitiza kuwa klabu kubwa kama Man Utd inahitaji na wachezaji bora, hivyo miongoni mwa washambuliaji waliopo kikosini hwatokuwa na budi kuonyesha uwezo wa kutoa msaada.

Kufuatia hatua hiyo inaonyesha dhahir safu ya ushambuliaji ya Man Utd itakabiliwa na ushindani wa kuwania nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kati ya Wayne Rooney, Robin van Parsie pamoja na Radamel Falcao.

Post a Comment