ROONEY AKABIDHIWA KITAMBAA CHA UNAHODHA ENGLAND
MSHAMBULIAJI
Wayne Rooney amekabidhiwa rasmi kitambaa cha Unahodha wa timu ya taifa
England na kocha Roy Hodgson jana kuahiria zama mpya Three Lions.
Kocha
wa England, Hodgson alitangaza wiki iliyopita kwamba Rooney atakuwa
Nahodha wake mpya kufuatia kiungo Steven Gerrard kustaafu soka ya
kimataifa.
England
inatarajiwa kumenyana na Norway katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa
kwenye Uwanja wa Wembley kabla ya kusafiri hadi Uswisi Jumatatu kwa
ajili ya mchezo wao wa ufunguzi wa kufuzu michuano ya Ulaya.
Rooney, ambaye sasa ana umri wa miaka 28, ameichezea mechi 95 England tangu aichezee kwa mara ya kwanza mwaka 2003.

Post a Comment