MWANAMKE AGONGWA NA DALADALA ENEO LA UBUNGO MAJI JIJINI DAR
Wasamalia wema wakijaribu kuokoa maisha ya dada aliyegongwa na gari (daladala) maeneo ya Ubungo maji wakati akivuka barabara.
Mwanamke
mmoja (jina halijafahamika) aliyekuwa anavuka barabara ya Morogoro
maeneo ya Ubungo maji kutoka ng'ambo ya tank na kuelekea upande wa
Tanesco amegongwa na gari ya daladala aina ya Toyota Coaster lililodaiwa
kuvunja sheria likiwa linapita kwenye barabara ya magari ya mwendo
kasi. Katika ajali hiyo dereva wa basi(daladala) hakupatikana kwani alikimbia baada ya ajali.
Majeruhi (dada huyo) akichukuliwa kwenye gari na wasamaria wema.
HiIi ndilo gari aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T454 BBV lililomgonga dada huyo.



Post a Comment