HIVI NDIVYO YANGA YA ILAZA THIKA UNITED YA KENYA BAO 1-0
MSHAMBULIAJI
mpya wa Yanga raia wa Brazili Geilson Santana Santos 'Jaja aliwatoa
wasiwasi mashabiki wa timu hiyo baada ya kufunga bao pekee lililoipa
ushindi timu yake wakati ilipopambana na Thika United ya Kenya leo
kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Huo
ulikuwa mchezo wa kwanza wa kirafiki wa kimataifa kwa Yanga inayo
nolewa na kocha Mbrazili Marcio Maximo,ambayo katika mchezo huo
ilionyesha kiwango cha kuvutia katika kipindi cha kwanza na kupoteza
nafasi nyingi za magoli sawa na wapinzani wao Thika Unite ambayo ilikuwa
ikicheza kwa kutegemea mashambulizi ya kustukiza zaidi.
Ushindi
huo unaifanya Yanga iliyomaliza nafasi ya pili msimu uliopita kucheza
mechi nne za kirafiki bila kupoteza hata mchezo mmoja baada ya awali
kuzifunga timu za Chipukizi,KMKM na Shangani za Zanzibar ilipokuwa
kwenye ziara ya siku 10 Visiwani humo.
.jpg)
Post a Comment