Hatima ya Bunge la Katiba mikononi mwa JK
Rais Jakaya Kikwete
Dodoma. Hatima ya Bunge Maalumu la Katiba
imebaki mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete, ambalo limemwandikia barua
kiongozi huyo wa nchi kutaka ufafanuzi wa kisheria kuhusu tarehe ya
mwisho ya kumaliza vikao vyake.
Hiyo ni kutokana na muda uliopangwa kwenye ratiba
ya bunge hilo kuzua utata wa kisheria na
kuwapo uwezekano wa mwingiliano na Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi (BLW), Zanzibar.
kuwapo uwezekano wa mwingiliano na Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi (BLW), Zanzibar.
Ratiba ya Bunge Maalumu la Katiba inaonyesha kuwa
limepanga kuhitimisha vikao vyake mwishoni mwa Oktoba, tofauti na tarehe
iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete Julai 28, mwaka huu ambayo
ilitangazwa katika Gazeti la Serikali (GN) namba 254 la Agosti Mosi.
Tangazo la Rais linaonyesha kuwa awamu ya pili ya
Bunge Maalumu ingeanza Agosti 5, 2014 na kumalizika Oktoba 4, lakini
ratiba ya Bunge hilo inaonyesha kuwa litamalizika Oktoba 31, siku ambayo
mwenyekiti wa Bunge hilo atakabidhi kwa Rais Katiba inayopendekezwa.
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa
hadi sasa Serikali bado haijatoa tangazo (GN) lingine kuongeza muda
hadi mwishoni mwa Oktoba kama alivyosema Mwenyekiti wa Bunge Maalumu,
Samuel Sitta wakati akitoa ufafanuzi wa siku 60 zilizotengwa kwa ajili
ya Bunge hilo, Agosti 5 mwaka huu.
Sitta alisema kwa kadiri ya tafsiri, siku za kazi
ni Jumatatu hadi Ijumaa ambazo wajumbe wanapaswa kufanya kazi na kwamba
Jumamosi na Jumapili siyo sehemu ya siku 60 zilizoongezwa na Rais.
Hata hivyo, Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis
Hamad alisema hadi sasa hawajapata maelekezo ya ziada kutoka serikalini
ambako waliandika barua ya kuomba ufafanuzi wa kisheria kuhusu suala
hilo.
“Tulimwandikia barua, Katibu Mkuu Kiongozi (Ombeni
Sefue) kuomba ufafanuzi wa siku hizo kama ambavyo sisi tungependa iwe,
lakini hadi sasa bado hatujajibiwa lakini bado siku zipo nadhani
tutajibiwa tu wakati mwafaka,” alisema Hamad ambaye pia ni Katibu wa
Baraza la Wawakilishi.
Sefue alikiri ofisi yake kupokea barua kutoka
Bunge Maalumu ikiomba ufafanuzi ambao ungeliwezesha kuongeza siku kwa
lengo la kukamilisha kazi ya kujadili na kuandika Katiba inayopendekezwa
na kwamba maombi yao bado yanafanyiwa kazi.
“Bado tuna muda wa kutosha tu, ni kweli
tulishayapokea maombi ya Bunge Maalumu kuhusu suala hilo na Mheshimiwa
Rais akikamilisha kazi yake watajulishwa tu,”alisema Sefue.
Utata wa kisheria
Licha ya ahadi iliyotolewa na Sitta ni dhahiri
kwamba suala hilo lina utata wa kisheria kutokana na kauli iliyowahi
kutolewa na Mwanasheria wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema wakati
akitoa ufafanuzi wa maana ya siku 70 ambazo Bunge lilikaa mara ya
kwanza.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI
Post a Comment