BECKHAM ASIKITISHWA KUMUONA WELBECK AKIONDOKA MANCHESTER UNITED

Mkongwe
wa klabu ya Manchester
United David Beckham anaamini kuwa ni huzuni kubwa kumuona Danny Welbeck
akiondoka ndani ya klabu ya Manchester United na anaamini kuwa usajili
huo ni moja kati ya usajili makini uliofanyika kwenye dirisha hili la
usajili la majira ya joto kwa kumjumuisha mshambuliaji huyo kikosini.

Welbeck,
mwemye umri wa miaka 23, amekamilisha uhamisho wa paundi milioni 16
siku ya mwisho ya usajili kutoka Manchester United kwenda Arsenal mara
baada ya bosi wa Manchester United Louis van Gaal kumwambia mchezaji
huyo kuwa anaweza kuenda atakako.

Beckham aliyeichezea England jumla ya michezo 115 na 58 kati ya hizo akiwa nahodha ameifungia Manchester jumla ya magoli
85 katika michezo 394 amesema hajisikii vizuri na anasikitika kumuona mshambuliaji huyo wa
Three Lions (Timu ya taifa ya Uingereza) akienda kumalizia karia yake ya soka nje ya Manchester United.
Post a Comment