HII KALI! MKE WA MCHUNGAJI AJIFUNGUA HIRIZI BAADA YA UJAUZITO WA MIEZI 7 HUKO BAGAMOYO
Wazee
wetu walishawahi kuneno kwamba; Ukishangaa ya Mussa utayaona ya
filauni! Ndivyo unavyoweza kuanza kusema kuhusiana na tukio la
kushangaza lililotokea Kijiji cha Udindila Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa
Pwani.
Mchungaji wa Kanisa la EAGT aliyetambulika kwa jina la Boniface Onesmo alijikuta akibubujikwa na machozi mara baada ya kushuhudia mkewe Bi. Benta Boniface akijifungua hirizi baada ya kushika mimba kwa kipindi cha miezi saba na nusu!
Akizungumza
na mtangazaji wa Kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm, Edson Mkisi
Jr, Mchungaji huyo alisema kabla ya kutokea kwa tukio hilo mkewe
amekuwa na matatizo ya kuharibika kwa mimba za mara kwa mara na tangu
kuhamia kwa eneo hilo la Udingila Bagamoyo mkewe huyo hajawahi kuzaa
mtoto hata mmoja ingawa amekuwa akishika mimba kila walipohitaji kuzaa.
“Kwa hakika Mungu ni mwema na sitaacha kuendelea kumsifu na kumuabudu,” alianza kueleza Mchungaji Onesmo.
“Zaidi
ya mtoto huyu mmoja niliyemzaa kabla ya kuhamia hapa, hivi sasa kila
ninapotaka kuzaa mtoto mimba za mke wangu zinaharibika na hadi muda huu
mimba zaidi ya nne zimeshaharibika na hii nyingine ndio amezaa hirizi!”
Mchungaji Onesmo alisimulia.
Aliezeza
kuwa siku ya tukio, mkewe kipenzi alianza kusikia uchungu tangu saa nne
asubuhi na kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo uchungu ulipozidi
kuongezeka.
“Hali
iliendelea hivyo hadi saa nne usiku ambapo mkewe alihisi kabisa kupushi
na mimi nilikuwa tayari kumsaidia lakini wakati anaendelea kupushi
mkewangu akawa anatoa haja ndogo mara kwa mara na alitoa haja ndogo hadi
ndoo nne ndogo zilijaa na kumwaga nje.
“Baada
ya hapo aliendelea kusikia maumivu makali ya tumboni huku akihisi kuzaa
lakini baadae aliposikia mtoto anakuja na mimi kujiweka tayari
kumzalisha niliona kitu kinatoka kama mtoto kukivuta ikatoka hirisi
ikiwa imefungwa kitambaa chenye rangi chekundu na nyeusi!” anasema.
Aidha, kwa upande wa mkewe, alisema kama siki hiyo kungekuwa na sumu ya panya angekunywa afe akapumzike.
Akizungumze
huku akilia, mama Dotto (Benta), anasema siku ya tukio hilo roho yake
ilinusa kaburi kama kama kungekuwa na hata mafuta ya taa kwenye kopo
angekunywa ili afe.
“Nilimuuliza
mume wangu mara kadhaa kama kwenye kopo kuna mafuta ya taa lakini
aliniambia yote aliweka kwenye kandiri (taa ya chemli) na hata
nilipoangalia tunapoweka sumu sikuiona….kwa hakika kama ningekiona
kimoja wapo ningekunywa nife! Nimetesema sana,” anasema mama Dotto.
Mama
Dotto alisema pamoja na changamoto zote anazokutana nazo Bagamoyo
lakini hajafikiria wala hafikirii kwenda kwa mganga wa kienyeji.
“Siwezi
kwenda kwa mganga wa kienyeji kwa sababu waganga ukienda wao huongeza
tatizo kwa hiyo nitaendelea kumuomba Mungu hadi atakaposikia maombi
yangu,” anasema huku akiangalia na mumewe pamoja na majirani waliofika
kumjulia hali.
Akizungumza
na Mkisi Jr, Mjumbe wa eneo hilo, Bw Hamza Adam, mbali na kuthibitisha
kufahamu kutokea kwa tukio hilo, pia alibainisha kwamba mbali na tukio
hilo ambalo hajawahi kukutana nalo tangu uhai wake, pia eneo hilo mifugo
imekuwa ikifa hovyo bila kuwepo kwa ugonjwa wowote.
Post a Comment