Yanga kujipima na Wakenya leo
![]() |
| Thika United |
BAADA
ya kupata ushindi katika mechi tatu mfululizo za kujipima nguvu dhidi
ya timu za visiwani Zanzibar, Yanga ya kocha Marcio Maximo itakuwa
kibaruani leo itakapowakabili Thika Utd ya Kenya.
Thika United inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya, imeshatua
jijini Dar tayari kwa mechi hiyo itakayokuwa ya kwanza ya
kwanza ya kirafiki ya kimataifa kwa Maximo.
Pia
ni mechi ya kwanza kwa Yanga na Maximo kucheza kwenye dimba la Taifa,
litakalotumika kwa mchezo huo ambao mashabiki wangependa kuona vipaji
vyao vipya vilivyosajiliwa na kukimbizwa Pemba kwenye kambi.
Baadhi
ya wachezaji wa Yanga wanaotarajiwa kuwa kivutio leo ni Geilson Santana
'Jaja' na ,Andrey Coutinho toka Brazil, Edward Charles na Said Juma
waliosajiliwa hivi karibuni pamoja na vifaa vingine vya zamani.


Post a Comment