Header Ads

Video: Wizkid aeleza chanzo cha Beef kati yake na Davido


Muimbaji wa Nigeria, Wizkid amezungumzia beef kati yake na
Davido akigusia kiini cha tofauti yao iliyokuzwa zaidi na comments za
mashabiki wao kwenye mitandao ya kijamii.



Wizkid amefunguka katika mahojiano aliyofanya na Olisa Abibua katika kipindi cha ‘The Truth’.



Ameeleza kuwa chanzo cha beef kati yao ni pale alipokuwa anatweet
akitoka kwenye show Marekani lakini tweet hiyo ilichukuliwa tofauti na
Davido aliyefikiria kuwa lilikuwa dongo kwake.



 Video: Wizkid aeleza chanzo cha Beef kati yake na Davido

Hivi ndivyo alivyoeleza:





“Ile situation ilikuwa ya kuchekesha kwangu kwa sababu tulikuwa
wote kwenye ndege moja. Nilirudi, nilikuwa natweet kweli kuhusu show
yangu, nilikuwa naongea kuhusu show yangu. Nilikuwa na show New York
kabla ya hapo, hiyo ilikuwa kama mwaka mmoja, miaka miwili iliyopita na
ilikuwa mbaya. Vyombo vya muziki vilikuwa vibaya, eneo lilikuwa la
ajabu…!




“Nilishuka uwanja wa ndege, nilikuwa naenda hotelini nilipofikia,
nikapitia kwenye eneo la show, nikaona jina langu kwenye taa
zinazongaa. Na nilikuwa ‘Wow’! Huyuni ni mimi!? “Nilishuka chini,
nikapita picha, nikapost nikisema nafanya show sahihi, kwenye maeneo
sahihi (I do Proper shows, proper venues). Watu wakaanza kuwaka na hisia
zao.”




Nilipoona hivyo, ilikuwa kichekesho. Wote ulikuwa mchezo, sipati
muda wala sina nguvu za kuomba. ‘show sahihi, eneo sahihi’ ndicho
ninachofanya. Sasa kama unakasirika, kwa nini unakasirika? Haufanyi show
sahihi kwenye maeneo sahihi? Nilikuwa siongei na wewe. Ninajisikia
hivyo kama nafanya kitu kwa ajili yangu, nafurahia mafanikio yangu na
unayachukia mafanikio yangu. Sijui cha kukwambia. Nikuchukulie kama
rafiki ama adui? Sijui.”




Wizkid ameeleza kuwa kama alikuwa amesema vile bila kuwataja watu
basi wasanii wote wa Nigeria wangechukizwa na kauli yake, na amehoji kwa
nini ilikuwa msanii mmoja tu aliyekasirishwa na tweet hiyo.

No comments

Powered by Blogger.