ROONEY AMTUNISHIA KIFUA FALCAO VITA YA NAMBA MAN UNITED
Hana hofu: Wayne Rooney anatumai ujio wa Radamel Falcao Manchester United ni jambo zuri
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amefurahia klabu yake Manchester United's kumsajili Radamel Falcao akisema ni mchezaji mzuri, lakini amesema hahofii kupokonywa namba.
Usajili
wa Falcao ndio lilikuwa tukio kubwa zaidi katika siku ya kufungwa pazia
la usajili, nyota huyo wa Colombia akitua United kwa mkopo wa Pauni
Milioni 6 kutoa huduma kikosi cha Louis van Gaal.
Lakini
Nahodha huyo wa United na England, Rooney hahofii ujio wa mchezaji huyo
kuhusu nafasi yake kikosini humo na anatarajia kucheza naye.
Pozi: Radamel Falcao akiwa ameshika jezi ya Manchester United baada ya kukamilisha uhamisho wake jana
Akizungumza
katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wa kirafiki wa
England dhidi ya Norway, Rooney amesema: "Sijui itaathiri vili nafasi
yangu, unatakiwa kumuuliza kocha,"alisema Rooney na kuongeza.
"Nafikiri ni usajili mzuri kwa kuwa ni mmoja wa wachezaji bora duniani," .

Post a Comment