MFANYABIASHARA AUAWA KINYAMA , ADAIWA KUFANYIWA NA MFANYABIASHARA MWENZAKE-SHINYANGA
| Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha |
Mfanyabiashara
mmoja aitwaye Mgaka Meleka(42) mkazi wa kata ya Mwakitolyo wilaya ya
Shinyanga vijijini amekutwa ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha
kali kwenye ubavu wake wa kushoto na kifuani upande wa kushoto na watu
wasiojulikana.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha tukio
hilo limetokea jana saa nne asubuhi katika kitongoji cha Kitalama katika
kijiji cha Mwakitolyo ambapo mwanamme huyo alikutwa ameuawa kwenye
kichaka nje kidogo ya kitongoji hicho.
Chanzo
cha tukio inasadikiwa kuwa marehemu alikuwa na ugomvi na mfanyabiashara
mwenzake aitwaye Balu Clement (35) mkazi wa Mwakitolyo.
Kamanda Kamugisha amesema mnamo tarehe 27,Agosti 2014 mtuhumiwa alikwenda dukani kwa marehemu na kutishia kumuua.
Mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi
source: Kadama Malunde-Shinyanga

Post a Comment