Header Ads

Video: Mkurugenzi wa Vodacom amwagiwa maji kuanzisha kampeni kuchangia Fistula #FistulaIcebucketChallenge






Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Rene Meza amekuwa wa kwanza kumwagiwa
maji ya barafu kwa lengo la kushiriki kampeni iliyoanzishwa na Vodacom

kuchangia akina mama wajawazito wenye ugonjwa wa Fistula
#IcebucketChallenge au #IceBongo.


 
Kampeni hii imenzishwa na Vodacom kwa kutumia mfano wa kampeni
maarufu iliyoanzishwa nchini Marekani kwa ajili ya kuchangia utafiti wa
matibabu ya ugonjwa wa ALS iliyopewa jina la ALS Ice bucket Challenge.
 
Mkurugenzi huyo wa Vodacom ameeleza kuwa wameamua kufanya hivyo kwa
kuchukua mfano wa ALS Challenge iliyoshika kasi kwenye mitandao ya
kijamii, kwa kuzingatia kuwa akina mama wajawazito zaidi ya 30,000
wanaugua ugonjwa wa Fistula kwa kukosa huduma bora za matibabu.
 
Amewataja (nominate) Naibu waziri wa Mawasiliano na Teknolojia,
January Makamba, Mkurugenzi wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez na
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Airtel, Sunil Colaso.

“You have 24 hours for the challenge or you pay $100 to support fistula in Tanzania.” Amesema.

No comments

Powered by Blogger.