DAKTARI AKUTWA NA MAITI DUKANI
Marehemu Jibuli Mahende, aliyepoteza maisha chini
Jeshi
la Polisi wilayani Ikungi, Singida linamshikilia daktari anayedaiwa
kuwa ni feki, Prosper Samson (pichani) kwa madai ya kumtibu mgonjwa
Jibuli Mahende, mkazi Kijiji cha Iyumbu, Sepuka na
kumsababishia kifo chake, Uwazi linakupa mkasa huo kwa kina.
kumsababishia kifo chake, Uwazi linakupa mkasa huo kwa kina.
Bw.Prosper Samson anayedaiwa kuwa ni daktari feki, akiwa nyumbani kwake.
Habari zinadai kuwa, Jibuli alifariki
dunia hivi karibuni baada ya kutibiwa na mtu huyo anayejiita daktari
kutokana na kile kilichodaiwa kuwa alizidishiwa dozi kwa kuongezewa
chupa tisa za maji ya drip sanjari na vidonge sita ambavyo
havikujulikana jina mara moja.
HISTORIA YA MAREHEMU
Kwa mujibu wa ndugu, marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua, kiuno na mgongo ambapo daktari huyo alimpa dawa hizo muda mfupi baadaye Jibuli alipoteza maisha akiwa kwenye duka la dawa, nyumbani kwa Prosper.

Bw.Prosper Samson akiwa chini ya ulinzi katika duka lake la dawa.
MGANGA MKUU WA WILAYA ASIMULIA
Akizungumza kwa niaba ya mganga mkuu wa Wilaya ya Ikungi, mmoja wa madaktari wa wilaya hiyo, Philip Kitundu alisema tukio hilo lilitokea juzikati saa nne asubuhi kwenye vyumba maalum vilivyotengwa na daktari huyo kwa ajili ya kutolea huduma mbalimbali za matibabu.

“Baada ya kupewa taarifa za kifo hicho
na utete wake, kesho yake tulikwenda kukagua duka la dawa la mtu huyo,”
alisema daktari huyo.
Kwa mujibu wa daktari huyo, walipofika
dukani kwa Prosper anayejitangaza kuwa ni daktari wa magonjwa ya
binadamu, walilikagua na kugundua kuwa hakuwa na leseni kutoka Mamlaka
ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) inayomruhusu kufanya biashara hiyo na
alikiri kuwa hakuwa na cheti cha chuo chochote alichosomea udaktari.
“Hata tulipopekuwa dukani kwake tulikuta
dawa ambazo haziruhusiwi kabisa kwenye maduka ya dawa muhimu, tulikuta
dawa na sindano na dawa za vidonda. Alikuwa anawafunga vidonda watu,
analaza na anatoa huduma za kujifungua kwa akina mama,” alifafanua
daktari huyo.
YADAIWA NI MTU WA TATU KUFA
Daktari huyo wa wilaya aliongeza kusema kwamba katika ukaguzi huo walikuta pia dawa zilizokwisha muda wake wa matumizi na kuwa tukio la Jibuli kupoteza maisha ni la tatu kwa watu waliopatiwa matibabu katika duka hilo, wawili walifia nje ya duka.

MTUHUMIWA ATOA MAELEZO
Kwa upande wake daktari huyo anayedaiwa ni feki, licha ya kukiri kumpokea mgonjwa huyo akiwa na hali mbaya na kwamba baada ya kuchukua historia yake aligundua alikuwa akisumbuliwa na kifua na kabla ya kupelekwa kwake alianza matibabu kwa waganga wa tiba asilia.

“Walikuja kwangu ili wapate ushauri
lakini jinsi nilivyomwona mgonjwa nikawashauri wafanye mikakati apelekwe
sehemu nyingine kwani niligundua ana matatizo tangu Juni, mwaka jana,”
alisema Prosper.
MTOTO WA MAREHEMU NAYE ANENA
Naye mtoto wa marehemu Jibuli aitwaye Jilala alisema siku ya tukio asubuhi alikwenda kumsalimia baba yake na kumkuta akiwa hoi, ndipo alipoamua kumpeleka kwenye duka hilo la dawa ambapo baada ya uchunguzi wa ‘daktari’ huyo aliambiwa baba yake alisumbuliwa na kifua, mgongo na kiuno.

“Baada ya dokta kunifahamisha ugonjwa
unaomsumbua baba, niliondoka kurudi nyumbani kutafuta fedha za kumuondoa
pale dukani ili kumpeleka Hospitali ya Mkoa wa Singida kwa matibabu
zaidi,” alifafanua mtoto huyo.
Akaendelea: “Hata hivyo, kabla ya baba
hajapoteza maisha alipokuwa dukani kwa dokta alipewa vidonge sita vya
dawa ambazo sikufahamu zinatibu ugonjwa gani na ilipofika saa nne
asubuhi alifariki dunia, nikamsusia na kuita watu kuja kuiona maiti ya
baba.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP Godfrey Kamwela amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP Godfrey Kamwela amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Post a Comment