YANGA YAVAMIA KAMBI YA SIMBA UNGUJA

Wachezaji
wa Simba wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuoni Chukwani mjini
Unguja jana Alhamisi kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara. Picha na
Mpiga Picha Wetu
SIMBA ipo Unguja chini ya Kocha Mzambia, Patrick Phiri, ikijipanga upya baada ya kupepesuka kwenye Ligi Kuu Bara msimu uliopita.
Wekundu
wa Msimbazi hao wamekuwa wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo uliopo
eneo la Chukwani pembeni kidogo ya mji wa Unguja.
Lakini huenda
wakashituka na kupigwa butwaa kwani Yanga ambayo inaishi kizungu zaidi
hapa Pemba, itahamishia kambi yao Unguja kuanzia kesho Jumamosi na
Jumapili watashuhudia 'live' mechi ya kirafiki ya Simba na timu ya
daraja la pili ya Kilimani City FC kwenye Uwanja wa Amaan.
Lakini hata Yanga na wenyewe wametangaza kwamba Jumapili watacheza hapohapo Unguja na KMKM ya Ligi Kuu Zanzibar. Kazi ipo.
Timu hizo zimekuwa zikikwepana kutokana na utani wa jadi ingawa kila moja ina hamu ya kusoma mbinu za mwenzake uwanjani.
Yanga
ipo Pemba tangu Jumatatu iliyopita na kocha wake Marcio Maximo amesema:
"Baada ya mazoezi ya kesho (leo Ijumaa), Jumamosi tutaondoka kwenda
Unguja ambako pia tutakaa kwa siku tano tutakakocheza pia mechi za
kujipima nguvu.
"Huku visiwani ni kutulia na mazoezi tu, hakuna mambo mengine yoyote tofauti na kama tungekaa Dar."
Ukifika
hapa Pemba kuna chimbo moja hatari sana linaitwa Misali ni kama
kilomita sita hivi kutoka mjini Chakechake kuna hoteli moja ya Kifahari
inaitwa Pemba Misali Sunset Beach.
Sehemu
kubwa ya majengo ya hoteli hiyo, imezungukwa na bahari hindi na miti
mirefu inayofanya mahali hapo kuwa tulivu na kama utasikia kelele, basi
lazima watakuwa ndege wa porini au mawimbi ya bahari.
Hapo
ndipo Mwanaspoti ilipoikuta Yanga ikifanya maandalizi yao ya mwisho ya
Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika. Mbali na yote kuna ufukwe
mzuri ambao unampa nafasi kila mchezaji anayetaka kufanya mazoezi yake
binafsi kujinafasi anavyotaka.
Maximo
amesema kambi hiyo ni ya ushindi kwani inawafanya wachezaji wake
watambue kwamba timu yao inaendeshwa kisasa na wao kazi yao ni
kudhihirisha hilo uwanjani na amepata 'First 11' mbili za hatari.
Katika
mahojiano na Mwanaspoti, Maximo amesema: "Timu ipo vizuri na kiwango cha
kila mchezaji kinafanana hali imesababisha nipate vikosi viwili ambavyo
ukivipambanisha na timu yoyote, nategemea kupata matokeo mazuri.
"Vikosi
hivyo ndivyo nitakavyovichezesha katika mechi zangu za kirafiki
nitakazocheza na itakapoanza ligi nitakuwa na timu yenye uwezo wa juu
kabisa."
Yanga
ilitarajia kucheza mechi ya kirafiki jana na Chipukizi ya Pemba baada ya
hapo itakwenda Unguja na kucheza tena Jumapili dhidi ya KMKM
inayofundishwa na kocha Ally Bushiri aliyewahi kufanya kazi na Maximo
enzi za Mbrazili huyo Taifa Stars.
Baada
ya mechi ya Jumapili, itaendelea na mazoezi hadi Jumatano ikapocheza
Shangani kabla ya kirudi Dar es Salaam na kucheza na timu mbili kali za
kimataifa.
"Nimezingatia
mlolongo mzima wa mazoezi ya kisasa na kisayansi hatuna hata majeruhi
isipokuwa Pato Ngonyani tu aliyegongana na mwenzake kwenye mazoezi na
kusababisha maumivu kwenye enka ya mguu wa kushoto," alisema Maximo.
"Yanga
inategemea mashabiki na ninachowaomba katika mechi hizo za kirafiki
wafike kwa wingi kuja kuiona timu yao. Kikosi chao kwa sasa kipo tayari
na mambo mengine ni marekebisho madogo madogo," alifafanua.
Katika
kambi ya Yanga ulinzi ni mkali kupita kiasi kwani ukionekana
hauelewekieleweki jirani na uwanja ambapo timu hiyo inafanya mazoezi
lazima utafukuzwa kwani bado usiri unatakiwa.
SOURCE:Mwanaspoti
Post a Comment