TETESI MPYA ZA USAJILI, ZIMEBAKI SIKU 10
Juventus na Roma wanataka kumsajili beki wa kati wa Manchester City
Matija Nastasic, 21, huku Newcastle na West Ham wakimtaka beki wa kulia
wa Man City Micah Richards, 26, (Manchester Evening News), Manchester
United wanaongoza mbio za kumsajili winga wa Real Madrid Angel Di Maria,
26 baada ya mabingwa wa Ufaransa PSG kuamua kujitoa (Daily Star),
lakini Di Maria huenda asiende United kwa sababu Louis van Gaal hataki
kukwaza ukuaji wa Adnan Januzaj, 19, (Daily
Express), Tottenham wanajiandaa kutoa pauni milioni 11 kumchukua
mshambuliaji wa QPR Loic Remy, 27, (Daily Star), Arsenal wanafikiria
kupanda dau kumchukua beki wa West Ham Winston Reid, 26, ambaye mkataba
wake unamalizika msimu ujao (Daily Star), Hull City wameongeza dau
kumchukua mshambuliaji wa Blackburn Jordan Rhodes, 24 (Daily Mail),
kiungo wa Manchester United Anderson, 26, huenda akahamia Sporting
Lisbon kwa pauni milioni 5.5 (Daily Express), boss wa Southampton Ronald
Koeman amesema kiungo wake Morgan Schneiderlin, 24 hauzwi kwa bei
yoyote (London Evening Standard), beki wa QPR Rio Ferdinand, 35, anataka
kuwa meneja wa England akistaafu kucheza (Daily Mail), Newcastle United
wana uhakika nahodha wao msaidizi Cheick Tiote, 28 hatoondoka licha ya
timu nyingi kumnyatia (Sunderland Echo), boss wa Arsenal Arsene Wenger
anaamini Jack Wilshere, 22, anatolewa kafara kwa England kushindwa
kufanya vizuri katika Kombe la Dunia (Sun), wakati huohuo Aaron Ramsey,
23, ana uhakika Arsenal wataweza kupambana "kwa misuli" na Manchester
City na Chelsea msimu huu (Sky Sports), Barcelona wamefanya jaribio la
kushangaza la kumtaka Angel Di Maria kutoka Real Madrid. Real
walifikiria dau la pauni milioni 48 lakini mazungumzo ya awali
yalivunjika baada ya Los Bloncos kutotaka kuwauzia mahasimu wao (Sport),
Napoli wanamtazama Fabio Borini wa Liverpool, ambaye kuwasili kwa Mario
Balotelli huenda kukasaidia kufanikisha uhamisho wake (Tuttosport), dau
la Manchester United kumtaka Nicolas Gaitan limekataliwa na Benfica
(Record), Arsenal wanafikiria kumchukua William Carvalho kutoka
Sporting, huku Sami Khedira anaweza kwenda Emirates iwapo atashusha
madai ya mshahara mkubwa (Daily Telegraph), AC Milan wanajiandaa kumtaka
mshambuliaji wa Tottenham Roberto Soldado kuziba pengo la Mario
Balotelli anayeelekea Liverpool. Spurs watamruhusu Soldado kuondoka na
nafasi yake kuzibwa na Loic Remy kutoka QPR (Daily Mail), Manchester
United na Zenit St Petersburg wapo tayari kupambana kumwania kiungo wa
Inter Milan Fredy Guarin (Corriere dello Sport), Barcelona wanatumaini
kukamilisha usajili wa Marco Reus kutoka Bayern Munich.
Maafisa wa Bayern wana wasiwasi kuwa huenda mchezaji huyo tayari amekubali kujiunga na Catalans ambao huenda wakafungiwa kusajili (Mundo Deportivo). Zimesalia siku 10 kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Maafisa wa Bayern wana wasiwasi kuwa huenda mchezaji huyo tayari amekubali kujiunga na Catalans ambao huenda wakafungiwa kusajili (Mundo Deportivo). Zimesalia siku 10 kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Post a Comment