TABIA MBAYA ZA VIONGOZI ZINAZOPELEKA KAMPUNI AU BIASHARA KUHARIBIKA.
Nimesikia
msemo unaosema watu huwa hawayaachi makampuni bali huwaacha mameneja au
huwakimbia mameneja wa makampuni hayo. Kam hivyo ni kweli, kuna baadhi ya
mameneja wanaweza kuwaweka watu ndani au kuwataabisha wafanyakazi wao.
Je tabia
gani mbaya ambazo zinakimbiza vipaji kwenye makampuni?
Kama uko
kwenye nafasi ya uongozi sasa huu ni wakati wa kutilia maanani hili mambo. Hapa
kuna baadhi ya tabia ambazo unatakiwa uondokane nazo kama unataka ubakie na
vipaji kwenye kampuni au shirika unaloliongoza ili liweze kufanikiwa.
1.
Kushindwa kuwasikiliza unaowaongoza
Je wewe huwasikiliza watu unaowaongoza wakileta wazo fulani kwako? Je unasikiliza mawazo yao wakati wa vikao?Je unajali wanachokiongea? Kwasababu unafanya kazi na watu wa tabia na hulka mbalimbali, inakupasa utilie maanani kila mambo ambalo linaletwa kwkao na kulifanyia kazi ipasavyo ili kuweza kusuluhisha na kupambana na changamoto kwenye kundi unaloliongoza. Kiongozi mzuri anajua kitu gani watu wake wanafanya, huchukua muda kuwasikiliza na wanapohitaji msaada huwa karibu yao kuwasaidia. Kushindwa kuwasikiliza kunasababisha msongo wa mawazo kwa watu unaowaongoza na watu hao hukosa tumaini juu ya viongozi wao kwenye kampuni au mashirika.
2. Kushindwa
kutumia vipaji ulivyonavyo kwenye kundi unaloliongoza
Kila timu
ina watu wenye vipaji tofauti tofauti , vipaji hivyo vinaweza muleta matokeo
mazuri kwenye kampuni na shirika kwa ujumla. Je wewe unajua vipaji ulivyonavyo
kwenye timu yako? Je umepata muda wa kuongea na kila mtu kujua namna ya kuweza
kumsaidia kutumia kipaji chake au ujuzi wake ipasavyo? Je umeweza kuongea na
kila mtu kujua uwezo alionao katika taaluma yenu kwenye biashara au shughuli
mnazozifanya? Kama umeshindwa kufanya hivyo unafanya kazi gizani sana.
Kiongozi
mzuri huhusisha watu wake na kutumia ujuzi na vipaji vyao kuleta matokeo bora
kwenye taasisi anayoiongoza. Kushindwa kufanya hivyo, huleta kukata tamaa kwa
wafanyakazi, kukosa motisha na kuzorota kiutendaji kazi.
3.
Kushindwa kutambua kazi za watu unaowaongoza
Je ni lini
uliwapongeza watu unaowaongoza? Je huwa unatambua juhudi zao kwa kusema
mafanikio na kumtambua kila mmoja anayefanya vyema kwenye kampuni yenu?
Kiongozi mzuri huchukua muda vile vile kutambua na kuwapongeza wanaofanya
vizuri kila wakati inapotokeo hivyo. Kushindwa kufanya hivyo kunahatarisha
kampuni na maendeleo yake.
4. Kuficha
Habari kwa unaowaoongoza
Je
unafanya nini kuhakikisha wanapata habari ya kila kinachoendelea? Je unatoa
mrejesho chanya na hasi pia kwa watu unaowaongoza? Je kama kuna tatizo kwa
mmojawapo kwenye kundi unashughulika nalo kivipi? Je unakusanya ushahidi wowote
kabla ya kufanya maaamuzi au unakurupukia kufanya maamuzi kabla ya kukusanya
ushahidi wa kutosha? Kiongozi mzuri ni mwaminifu kwa watu anaowaongoza kwa
kuwapa habari kwa usahihi na kurekebisha panapostahili, hapo inapohusisha
wafanyakazi hao.
Kushindwa
kuwasiliana vizuri na timu yako kuna madhara kiutendaji na mafanikio yenu.
5. Je
unatoa majibu?
Je huwa
unajibu swali au unapindisha majibu ya swali pale wafanyakazi wanapohitaji
majibu? kama hauko tayari kutoa majibu ya msingi kwa wale unaowaongoza, nao
wanakata mawasiliano na wewe kwa kuwa huna msaada kwao.
6. Kuwa
mtemi
Je wewe ni
mtemi katika maamuzi, mawazo na utendaji? Je wewe unazuia watu unaowaongoza
kuwafikia viongozi wa juu? Kama wewe ni mtemi unayefanya watu wakuogope,
haitakusaidia kufanya vyema kwenye kiting chako.
7. Kuwa na
visasi au hasira
Inawezekana
mmoja wa wale unaowaongoza hajakubaliana na wazo lako au kile ulichowasilisha
au hata maamuzi uliyofanya. Je unachukua hayo maamuzi kwa hasira au kutafuta
namna ya kumkomesha? Kama unafanya hivyo wewe hiyo sio tabia nzuri hasa kama
wewe ni kiongozi. Kiongozi mzuri anakubali rejea kutoka kwa watu anaowaongoza
inapokua nzuri au mbaya. Kampuni inaongozwa vyema pale kila mmoja anapowajibika
ipasavyo, pale unapozuia watu unaowaongoza kutoa sauti zao hawakuamini wala
kukuthamini kama kiongozi wao.
8.
Unyanyasaji au matumizi ya nguvu kihisia
Inawezeka
huwapigi kwa ngumi bali namna gani unatumia nafasi yako kama kiongozi wao? Je
kihisia unawafanyia nini wafanyakazi wake? Je unawaheshimu wafanyakazi wako?
Kama kiongozi unatakiwa kuwaheshimu wafanyakazi wake au watu unaowaongoza kihisia,
kitaaluma na hata muonekano wao, hivyo unatakiwa kutofautisha mambo ya kikazi
na binafsi kwao ili kuboresha mahusiano nao.
Je wewe
huwa unafanya mini? Unachotakiwa kujua kila unachokifanya huharibu kampuni au
taasisi taratibu bila ya wewe kujua. Siku moja utakuta kampuni yako haipo tena
au taasisi inapata shida kiutendaji na unatafuta mtu wa kumlaumu. Una nguvu ya
kuhakikisha kampuni au taasisi inakwenda juu au chino kila kitu kilo mikononi
mwako.
Chanzo: Bongo5
Post a Comment