TAARIFA NJEMA: FURAHA YAKARIBIA KUREJEA MANCHESTER UNITED.
Jana
Meneja wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti alithibitisha taarifa
zilizokua zimzagaa jijini Madrid kuwa wachzaji wawili hao wamegoma
kuongeza mkataba na mabingwa hao wa Ulaya na hivyo kuthibitisha kuwa
wachezaji hao wawili wanaweza kuondoka kwenye majira haya ya kiangazi
kabla ya dirisha la usajiri kufungwa.

Gazti la The Manchester Evening News
limandika kuwa Meneja wa timu hiyo Louis van Gaal anatarajiwa kujaribu
bahati yake kwa kujaribu kuwasajiri Khedira na Di Maria kwa wakati mmoja
kutoka Madrid.
Wadadisi
wa mambo wanadai kuwa klabu ya Real Madrid wako tayari kuikubali ofa
yoyote itakayokua inazidi paundi milioni 20 kwaajili ya Sami Khedira.
Lakini pia
ikumbukwe kuwa makamu mwenyekiti wa klabu ya Manchester United Ed
Woodward tayari alikwishaanza kufanya mazungumzo na mabosi wenzake wa
Real Madrid yenye lengo ya kukamilisha dili la paundi milioni 50
kwaajili ya kumnasa Di Maria.
Endapo
usajiri huu utakamilika unaweza kurejesha furaha kwa mashabiki wa
Manchester United ambao wanaonekana kukasirishwa na mwenndo mbaya wa
usajili wa klabu hiyo.

Taarifa
njema kwa mashabiki wa klabu hiyo ni kurejea mazoezini kwa mshambuliaji
wake tegemezi Robin van Persie akijiandaa kwaajili ya mchezo wa Barclays
Premier League dhidi ya Sunderland siku ya jumaapili.
Post a Comment