MTOTO AUAWA KWA KUBAKWA KISHA KUTOBOLEWA MACHO
Mtoto
aitwaye Happiness Kashindye mwenye umri wa miaka 9 mwanafunzi wa darasa
la tatu katika shule ya msingi Negezi iliyopo kata ya Ndala Manispaa ya
Shinyanga ameuawa kikatili kwa kubakwa
kisha kutobolewa macho na watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa
kichakani.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana saa saba mchana katika kitongoji cha Kashampa kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi ambapo mwili wa marehemu ulikutwa kichakani.
Kaimu mganga mfawidhi wa
hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Dkt Daniel Maguja amesema vipimo vinaonesha kuwa mtoto huyo alibakwa na kutobolewa macho.
Kamanda
wa polisi mkoani hapa Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kuongeza kuwa chanzo cha tukio
hilo kinachunguzwa huku akitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa
zitakazosaidia kuwabaini na kuwakamata wauaji ili hatua za kisheria
zichukuliwe.
Post a Comment