MFANYABIASHARA WA MADINI AJIPIGA RISASI, KUAKIKWEPA ASIUAWE NA WANANCHI WENYE HASIRA
MFANYABIASHARA
maarufu wa madini ya dhahabu amejiua kwa kujipiga risasi kichwani.
Amefanya hivyo wakati akiwakimbia wananchi wenye hasira na wachimbaji
wadogo kwenye machimbo ya Kalole Kata ya Bugarama wilaya ya Kahama,
baada ya kumjeruhi mguuni kwa kumpiga risasi mchimbaji mdogo wa machimbo
hayo.
Kamanda
wa Polisi, Mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alisema ofisini kwake
mjini hapa jana kuwa tukio hilo ni la juzi saa 12 jioni kwenye machimbo
hayo.
Alimtaja
mfanyabiashara huyo ni Mwigulu David (34) na kwamba inadaiwa alikuwa
akiwadai wafanyabiashara wenzake mgawo wake wa dhahabu, waliyowapunja
wachimbaji.
''Katika
purukushani hiyo, Mwigulu alikuwa akimhoji mmoja wa wafanyabiashara
wenzake katika mzozo wa kugawana dhahabu waliyowapunja wachimbaji,” alisema Kamanda.
Kamanda alisema,
“Mwigulu alichomoa bastola yake kutoka mfukoni kwa lengo la kutaka
kumshambulia mmoja wa wafanyabiashara wenzake na kwa bahati mbaya risasi
ikamjeruhi kwenye mguu wa kushoto mchimbaji Maduhu Amos (25) na
kusababisha akimbizwe hospitali kwa matibabu.''
Kutokana na kitendo hicho, wananchi wakiwemo wachimbaji wadogo walimzonga mfanyabiashara huyo.
Inadaiwa
alipoona hali imebadilika huku watu wengi wakitaka kumpiga, aliingia
kwenye gari lake na kuliondoa kwa kasi, akitaka kujinusuru kwa kipigo
cha wananchi wenye hasira.
Akiwa
njiani alikuta barabara kuu, inayotoka kwenye machimbo hayo kwenda
mjini Kahama ikiwa imezibwa kwa kuwekewa magogo na mawe makubwa huku
gari likishambuliwa kwa mawe kutoka pande zote.
“Aliamua
kuteremka kwenye gari na kukimbilia kwenye moja ya nyumba zilizopo
kando ya barabara hiyo na kujifungia, lakini hata hivyo wananchi
waliokuwa wakikimbiza gari hilo waliendelea kurusha mawe na kutishia
kuvunja milango na kuichoma moto nyumba hiyo,” alisema kamanda.
Kulingana
na maelezo ya kamanda, Mwigulu akiwa amejifungia aliamua kujipiga
risasi tatu kichwani zilizosababisha kifo chake papo hapo.
Post a Comment