Header Ads

Mashabiki wamuuwa mcheza mpira Algeria

Timu ya Algeria ilipoishinda Urusi katika kombe la Dunia Brazil
Mchezaji mpira kutoka Cameroon amekufa baada ya kupigwa kichwani wakati mashabiki waliokereka waliporusha mawe mwisho wa mechi ya ligi ya Algeria.
Albert Ebosse, aliyekuwa na umri wa miaka 24, ndiye aliyetia magoli mengi kabisa katika ligi ya Algeria msimu uliopita.
Alirushiwa kitu wakati mashabiki walipokerwa kuwa timu yake, JS Kabylie, iliposhindwa kwa magoli mawili kwa moja katika mechi iliyochezwa nyumbani, Tizi Ouzou.
Yeye ndiye aliyepata hilo goli moja kwa timu yake.
Wizara ya mambo ya nchi ya Algeria imeamrisha uchunguzi ufanywe.
Ligi ya Algeria imefunga uwanja wa mpira wa timu ya JS Kabylie na imeitisha mkutano wa dharura Jumatatu.

SOUCRE: BBC

BAADA YA KUNDI LA ORIJINO KOMEDI KUDAIWA KUSAMBARATIKA HII NDO KAULI YA MASANJA MKANDAMIZAJI


Baada ya miaka kadhaa ya kutamba kwa kundi la
vichekesho la Ze Komedi kisha kudaiwa
kusambaratika, mmoja wa memba wa kundi hilo,
Emmanuel Mgaya ‘ Masanja Mkandamizaji’ ameibuka
na kueleza kutokana na ishu nzima.
Masanja ambaye pia ni mchungaji amefunguka na
kueleza kila kitu kuhusiana na ishu hiyo huku
akikanisha vikali kuwepo kwa ufunjifu wa kundi hilo.
Akizungumza na mwandishi wetu, Masanja alisema
kuwa kundi hilo halijavunjika kama ilivyoripotiwa na
kudai kuwa litarejea kama kawaida kuanzia mwezi
Septemba mwaka huu na kuendelea kubamba kama
ilivyozoeleka kipindi cha nyuma na kufanikiwa kujizolea
umaarufu wa kutosha nchini.
“Kikubwa tu watu waachane na hizo tetesi Ze Komedi
kwamba imevunjika, nasema kwamba haijavunjika
wala hatujasambaratika hata kidogo, tupo na
tutaendelea kuwepo. Rasmi tutaanza kazi Septemba
mwaka huu,” alisema Masanja.
- See more at: http://mwanaharakatimzalendo.blogspot.com/2014/08/baada-ya-kundi-la-orijino-komedi.html#.U_n1yleqDrQ

No comments

Powered by Blogger.