Hatimaye Di Maria rasmi Man Utd

HATIMAYE Muargentina, Angel Di Maria ametua na kusaini
mkataba wa miaka mitano kuichezea Manchester United.
Atakuwa akilamba mshahara wa pauni 200,000
kwa wiki, anachukua nafasi ya pili kwa mshahara mkubwa baada ya nahodha wake,
Wayne Rooney.
Mchezaji
huyo hata hivyo aliingia Old Trafford na mguu mbaya baada ya klabu yake
hiyo kulambwa mabao 4-0 na timu ya Daraja la Kwanza katika mechi ya
Kombe la Ligi na anategemea kuwemo katika kikosi cha Mashetani hao
Wekundu katika mechi ya Ligi Kuu siku ya Jumamosi dhidiya Banley.
Post a Comment