Hatari!! Jokate, Vanessa Mdee Katika Beef Zito Kisa Penzi La Ommy Dimpoz
Habari ya Mjini ni kuhusu Jokate Mwegelo kutoka kimapenzi na Ommy Dimpoz ambaye ni star wa Bongofleva.
Habari
 zaidi zinasema kuwa Jokate na Ommy Dimpoz wamekuwa wapenzi kwa muda 
sasa ila kwa siri kubwa ikidaiwa wote hawakuwa tayari kuweka uhusiano 
wao hadharani wakiogopa media kuanza kuwafuatilia.
Inadaiwa
 pia kuwa Ommy alikuwa anatoka kimapenzi na Vanessa Mdee lakini baada ya
 Vanesa kugundua kuwa Jokate anamzunguka zikawa haziivi tena na 
huchekeana kinafiki tu wakikutana .
Kwasasa
 Jokate na Ommy wanaliendeleza libeneke la huba kwa siri.Habari 
zinaingia ndani zaidi kwa kusema kuwa Jokate alikuwa pia akienda 
mikocheni alipodaiwa alikuwa nakaa Dimpoz sababu ya penzi kukolea.
Hata hivyo si Jokate, Ommy wala Vanessa ambaye amepatikana kuzungumzia suala hili.
 
 


 
 
 
 
Post a Comment