Header Ads

EXCLUSIVEE::::: HAYA NDIO MAAMUZI YA TCRA JUU YA REDIO CLOUDS FM BAADA YA KIKAO LEO,SOMA HAPA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgXIdPmsrgNhjFmWdFyw_Z-iXnbK8Np2uMfSXzEMs0uQoLtfPEwnQuJg2_GUR3IDvkmJ1BrB5zEUOL7ittnaWNuuJUZ-zOUrH20cD-KU6SPPG6mOotYsra5BKCg3ZM45wDNwLStfY-Ngh4/s1600/TC.jpg

 

 

 


 

 

 

 

 

 

 

 

 


EXCLUSIVEE::::: HAYA NDIO MAAMUZI YA TCRA JUU YA REDIO CLOUDS FM BAADA YA KIKAO LEO,SOMA HAPA

walikuwa wakiyaamini yalikuwa siyo ya kweli na hayapo. Mila hizi potofu mwisho wa siku zitasababisha mgonjwa asiende hospitali. 5.2 Maelezo ya Bwana Ruge Mutahaba Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Entertainment FM Bwana Ruge Mutahaba alitoa utetezi wake kwa kusema changamoto kubwa inayokikabili kituo chake ni kutafuta ubunifu wa kuwafikia walengwa ambao ni vijana. Bwana Ruge alisema maneno yafuatayo:-
“…..ukisikiliza kipindi cha Njia Panda siku zote kimekuwa kinazungumza kuhusu…. an individual person….
na story yake na namna alivyokutana na jambo lililogeuza maisha yake na jambo hilo mwisho wa siku
lilivyo muathiri kuelekea kupata maambukizi….”
 Bwana Ruge aliendelea kusema kwamba kituo chake kilianzisha kampeni ya Vunja Ukimya ambayo ilikuwa na lengo la kuzungumzia HIV kwa uwazi na kuleta vijana wengi ambao walijitangaza kuathirika na ugonjwa wa Ukimwi ilikuisaidia jamii. Alisema kipindi kilicholalamikiwa kilihitimishwa kwa kuelezea mambo yanayohusu uchawi na ushirikina hayana msaada wowote. Bwana Ruge alisisitiza kwamba kipindi kiliruka kwa wiki tatu. Mhusika alianza kuzungumzia maisha yake ya kawaida, akaenda kwenye sehemu ya pili ya kuingia kwenye misukule na akaenda kwenye sehemu ya tatu akazungumza kwamba hata ile ajali na matukio yaliyotokea ilikuwa ni ajali ya kawaida kama nyingine zinavyotokea na kwamba yeye hana nguvu hiyo na hayo mambo siyo ya kweli.
Bwana Ruge alisema huyu aliyekuwa anasimulia ni mtu mpumbavu yaani “ Stupid” na aliyoyasema
yalikuwa siyo ya kweli. Alisema maneno yafuatayo:
“ ……hakuna aliyesema wale walikufa kwa kulogwa….tunachozungumza ni kwamba there is a stupid
 guy
alikuja kusema amehusika na hii kitu….this guy is a stupid guy lakini mwisho wa siku inakuja kujulikana ni uongo……”
Bwana Ruge alisema waliamua kuweka masimulizi hayo kwa sababu watu wanaamini vitu ambavyo havipo kwenye jamii.

 

 6.0 Kukiri Kosa Mkurugenzi wa Clouds Entertainment FM Bwana Ruge Mutahaba alisema kwamba hawakufanya kosa lolote na hitimisho la kipindi katika wiki ya tatu lilieleza kwamba mambo yaliyosemwa ni ya uongo na hakuna kitu kama hicho. 7.0 Tathmini ya Kamati Kamati iliridhika na kusisitiza kwamba, kituo cha Clouds Entertainment FM Radio katika kipindi cha Njia Panda kilikiuka Kanuni za Utangazaji kwa kutangaza maudhui yenye simulizi za kishirikina na kichawi  jambo ambalo ni kinyume na taratibu na Sheria za nchi. Habari na simulizi za Safari ya Kuzimu zinaweza kupelekea kuipotosha jamii na ni kinyume na utamaduni wa Taifa. Jambo hili linaweza kumomonyoa utaifa wa Watanzania, vilevile linaweza kuumiza hisia za wananchi wa Tanzania na kusababisha mvurugano miongoni mwa wananchi, pamoja na kuhatarisha usalama wa taifa. Kitendo hiki ni kinyume na Kanuni za Utangazaji (Maudhui).


Vilevile, lugha iliyotumika kuendesha kipindi hicho ilikuwa ni ya moja kwa moja isiyopunguza ukali wa

maneno badala ya kutumia “tafsida”. Lugha

 iliyotumika ni lugha inayoweza kuwajengea hofu wasikilizaji, na inaweza kuwajengea watoto tabia mbaya na kuwapotosha kutokana na kusikia mambo yasiyofaa. Jambo hili ni kinyume na Kanuni za Utangazaji (Maudhui),2005, 8.0 Uamuzi wa Kamati Kamati iliridh

ika kuwa kipindi cha “Njia Panda” kilichorushwa hewani na kituo cha Clouds Entertainment

FM Radio tarehe 15/06/2014 kilikiuka Kanuni za Utangazaji, 2005 Na. Na. 5(a), (b), (c), (d), (f), (g), (h), 14(1), 15(b) na 22(1),(3),(a),(b):- kama ilivyonukuliwa hapo juu.

Baada ya kusikiliza na kutafakari kwa kina maelezo ya utetezi kutoka kwa Mkurugenzi wa Vipindi wa
Clouds Entertainment FM Radio na Mtangazaji wa kipindi cha “Njia Panda”, Kamati ya Maudhui inaamua
yafuatayo:- 1.1 Clouds Entertainment FM Radio inapewa onyo kali; na, 1.2 Clouds Entertainment FM Radio inatozwa faini ya shilingi milioni nne za Kitanzania ambazo inapaswa kuzilipa kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ndani ya mwezi mmoja toka siku ya uamuzi huu. Endapo Clouds Entertainment FM Radio itakiuka tena Kanuni za Utangazaji, hatua kali zaidi za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Uamuzi huu umetolewa na kusomwa Dar es Salaam siku hii ya ……., Mwezi wa Agosti Mwaka 2014.
 Haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu iko wazi ndani ya siku 30 tangu uamuzi unapotolewa Uamuzi Umesainiwa na: Eng. Margaret T. Munyagi
………………………………......
 (Sahihi) Mwenyekiti WAJUMBE WA KAMATI YA MAUDHUI 1. Bwana Walter Bgoya (Sahihi)....................................... 2. Bwana Joseph Mapunda (Sahihi).................................
3. Bwana Abdul Ramadhani Ngarawa

No comments

Powered by Blogger.