BALOTELLI ATUA RASIMI LIVERPOOL KUKAMILISHA USAJILI WAKE
MSHAMBULIAJI
Mario Balotelli alitarajiwa kuwasili England leo mchana kwa ajili ya
kufikia makubaliano ya kujiunga na Liverpool baada ya klabu hiyo
kufikia makubaliano na wawakilishi wake.
Mpachika
mabao huyo wa zamani wa Manchester City yuko karibu kusaini kikosi cha
Brendan Rodgers na amekwenda huko kukamilisha dili hilo mara moja.
Baada ya
kuwasili, Balotelli alitarajiwa kwenda kufanyiwa vipimo katika hospitali
ya klabu hiyo, Spire Liverpool kabla ya kwenda kufanyiwa vipimo zaidi
vya afya katika viwanja vya Melwood vinavyotumika kwa mazoezi na klabu
hiyo.
Pamoja na
hayo, mshambuliaji huyo wa Italia hataweza kuichezea Liverpool dhidi ya
klabu yake ya zamani, Manchester City Jumatatu usiku, katokana na muda
wa usajili kwa leo kupita.
Anawasili: Mario Balotelli aliyepigwa picha hii mwaka jana, anatua Liverpool leo kukamilisha usajili wake.
Post a Comment