BABY MADAHA, WYRE WA KENYA WAKOLEA KIMAPENZI KWA
Mwanadada anayefanya vizuri katika muziki Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ akipozi na Kevin Wyre.
Shani Ramadhani MWANADADA
anayefanya vizuri katika muziki Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby
Madaha’ kwa sasa amejiweka kimapenzi na msanii anayetamba Kenya, Kevin
Wyre baada ya kuwepo kwa tetesi za kutemana na mtu wake wa awali, Joe
Kairuki aliyekuwa pia ni meneja wake.
Watu walio karibu na
wawili hao wanasema uhusiano huo unafanywa kwa siri ili usivuje na
kwamba kwa sasa pia wanafanya kazi ya pamoja itakayokuwa hewani wakati
wowote muda mfupi ujao.
Alipoulizwa
juu ya ishu hiyo, Baby Madaha alitiririka: “Mimi nina uhuru wa kufanya
chochote ninachojisikia na hakuna mtu atakayeweza kuniingilia katika
maisha yangu wala uhusiano wangu kwa sababu sigongi kwa mtu kuomba
msaada.”

Post a Comment