ANGEL DI MARIA ANUKIA MANCHESTER UNITED BAADA YA KUTOSWA KIKOSI CHA JANA REAL MADRID IKICHARAZWA 1-0

Aliachwa: Angel Di Maria hakupangwa katika kikosi cha Real Madrid kilichokabiliana na Atletico Madrid jana usiku.
CARLO
Ancelotti amethibitisha kuwa mchezaji anayewaniwa kwa nguvu zote na
Manchester United, Angel Di Maria aliachwa katika kikosi cha jana kwenye
mchezo wa marudiano wa Spanish Super Cup dhidi ya mahasimu wake,
Atletico Madrid na kupoteza kombe la kwanza msimu huu kwa sababu za
kimpira na si vinginevyo.
"Aliachwa katika kikosi kwa sababu za
kimpira" Alisema Ancelotti alipoulizwa kwanini hajampanga Muargentina
huyo hata katika orodha ya wachezaji wa akiba jana uwanja wa Vicente
Calderon.
Kitendo cha Di Maria kutopangwa jana
kinaashiria uhusiano na kocha Ancelotti umefikia hali mbaya na ni sababu
tosha kwa Manchester United kumnasa kwa ada inayoaminika kuwa paundi
milioni 50.
Ancelotti alithibitisha kuwa nyota huyo
wa Argentina katika fainali za kombe la Dunia majira ya kiangazi mwaka
huu ameomba kuondoka Real Madrid.

Mashabiki wa Real Madrid wameiacha klabu katika wasiwasi kwasababu wanamhitaji Di Maria kubakia, lakini Rais Florentino Perez anataka auzwe ili kuweka sawa mahesabu baada ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kumsajili Toni Kroos na James Rodrgiguez.
Madrid walibaki katika utata mkubwa
kutokana na mashabiki waliohudhuria Santiago Bernabeu siku ya jumanne
kulipuka kwa shangwe wakimshangilia Di Maria baada ya kuingia uwanjani
kipindi cha pili akitokea benchi.
Ancelotti alithibitisha ijumaa kuwa mchezaji amekataa kusaini mkataba mpya na ameomba kuondoka.
Post a Comment