AMBURUZA MAHAKAMANI ASKOFU WA SHINYANGA ANAYEDAI KUWAFUKUZA WACHUNGAJI WA KANISA BILA MAKOSA
Waumini wa kanisa la EAGT Majengo mjini Shinyanga wakiwa
katika mahakama ya wilaya ya Shinyanga wakiwa wameshikilia
mabango
Kesi inayomkabili Askofu wa Kanisa la
(EAGT) , kanda ya Magharibi Rafaeli Machimu,Dhidi ya waumini wa dhehebu hilo
lililopo Majengo Mjini Shinyanga ,kwa madai ya kuwanyanyasa kwa kumfukuza
Mchungaji wao David Mabushi bila kosa lolote ambaye bado wanamuhitaji imeanza
kusikilizwa mahakamani.
Kesi hiyo imeanza kusikilizwa jana katika
mahakama ya wilaya ya Shinyanga,lakini mahakama imeahirisha shauri la kesi
hiyo, lililofunguliwa na waumini baada kuona upande wa mlalamikaji haukukidhi
vigezo vya sababu ya kufungua shauri hilo.
Akisoma shauri ya kesi hiyo hakimu mwandamizi wa wilaya Thomson Mtani
katika mahakama hiyo alisema mahakama imeona kwa upande wa mlalamikaji kuwa
shauri dogo namba 08/2014 lililofunguliwa kupitia kwa mwanasheria Norbat Beda
halina sababu ya kufunguliwa kwake.
Hakimu Mtani alimuomba wakili wa upande wa
mlalamikaji Norbat Beda aandike upya sababu za msingi za kufungua kesi hiyo,
ili wakili wa upande wa pili wa mlalamikiwa Bartazar Mwairo aweze kujibu haraka
shtaka hilo dhidi ya mteja wake siku ya kesi iliyopangwa kusikilizwa tena Agoust
28 mwaka huu.
Shauri hilo lililokuwa linapinga kitendo cha Askofu wa kanisa la
EAGT kanda ya Magharibi kumwandikia barua ya kumfukuza mchungaji Mabushi katika
kanisa hilo itasomwa tena agosti 28 mwaka huu
Aidha kesi hiyo ilianza kutajwa tarehe 4 Agosti ,2014, katika
mahakama ya wilaya na mara
ya pili ilisikilizwa Agosti 14, na kuahirishwa kusikilizwa kwa sababu wakili wa
mshitakiwa aliiomba mahakama iahirishe kusikilizwa kutokana na kutoelewa kina
cha kesi hiyo hivyo ilitarajiwa kusikilizwa tena Agosti 25 imeahirishwa tena mpaka Agosti
28 mwaka huu.
Waumini wa kanisa hilo walimfikisha mahakamani Askofu Rafael Machimu Agost
4 mwaka huu, kwa madai ya kuwanyanyasa kwa kuwafukuza mara kwa mara wachungaji
wa kanisa lao la( EAGT),la Majengo Mjini Shinyanga bila ya Sababu za msingi.
Walisema kanisa hilo lilianzishwa mwaka 1992 likiwa chini ya mchungaji John
Chambi ambaye aliondolewa na uongozi wa jimbo la Shinyanga akiwepo mchungaji
Rafael Machimu ambaye wakati huo alikuwa katibu wa jimbo hilo.
Waumini hao walisema tangu mwaka huo waliendelea kuabudu bila mchungaji
hadi mwaka 1999 kanisa hilo lilipelekewa mchungaji Mothes Kuzenza ambaye kwa
sasa ni marehemu naye aliondolewa mwaka 2003 katika mazingira ya kutatanisha.
Walisema walivyofuatilia waligundua kuwa ameondolewa kupitia mkono wa
Askofu Rafael Machimu ambaye wakati huo alikuwa katibu wa kanda, na kudai
wamechoka kuona wachungaji wao wakiondolewa mara kwa mara bila ya makosa.
“Kwa kweli tumechoka kuondolewa ondolewa wachungaji mara kwa mara tumeamua
sasa kwenda katika ngazi ya mahakama tuone kama mchungaji wetu Mabushi kama
atakuwa na makosa ya kuondolewa katika kanisa la majengo,”.
“Sisi ndiyo waumini wa hili kanisa na ni waumini wa miaka mingi hakuna mali
ya EAGT hata bati moja haijaleta, mali iliyopo humo ni mali ya waumini na hatu
taki kunyanyaswa bado tunamhija mchungaji wetu David Mabushi”,walisema
waumini hao.
Post a Comment