Header Ads

AFYA: MATUNDA NA FAIDA ZAKE MWILINI

AFRIKA imejaaliwa mimea, madini, rutuba na hali ya hewa safi, ikiwa ni urithi tangu enzi na enzi.
Pamoja na bara hili kujaa vyakula vyote vinavyohitajika na wanadamu, bado uhai wa watu wake wengi ni mfupi.
Katika orodha ya wastani wa maisha iliyowahi kutolewa na Shirika la Ujasusi Marekani (CIA) na Umoja wa Mataifa (UN) mwaka 2011, nchi zinazoongoza kwa maisha marefu ni Japan.
Wajapani wanaishi hadi miaka 90 na kuendelea, Ulaya, Marekani na China kati ya 75 hadi 90, nchi za bara Asia mathalan India wanaishi miaka 65 na Tanzania ikiwekwa katika wastani wa miaka 50 hadi 53.
Wajapani wanasifika kwa kula vyema, hawali vyakula vyenye mapishi ya mambo mengi, ulaji wao ni mdogo mdogo, wa mara kwa mara, hawajazi sana matumbo na siri yao kubwa ni ulaji wa vyakula ambavyo husaidia kukarabati na kuhifadhi mwili, ikiwemo mimea ya baharini.
Mmea mkubwa ambao Wajapani uhutumia unaitwa Kombu ambao unachemshwa na kutumia maji yake kwa kupikia mchuzi, chai na uji.
Moja ya faida ya Kombu ni kukinga na kuuponyesha mwili kutokana na maradhi, kuongeza nguvu za nywele, ngozi na maisha na ndiyo sababu hasa wataalamu wanaeleza kuwa ni nadra kumwona Mjapani asiyekuwa na nywele nyingi.

 Vitu vinavyosaidia mwili

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiGH85KoS_ghICSlpSYbFAfmq-hB8WGvVgXjfat_F1e8ITzlIG_66wWX09WPPT5ZJxQB1EYzjZ2xhwMQ5HQY1l0P0iZBLew_iMlb-telxZIRZ69XRFlAe9auoAIsGXvMOzQrfbxDVyoWRUM/s1600/BOGA.jpg

Mbegu mbichi za maboga zina faida sana mwilini; kwa kutoa mafuta asilia yasiyodhuru moyo, kutoa kinga ya maradhi, ujenzi na kukarabati ngozi, mifupa, kucha, nywele, kuupa mwili nguvu za rijali.
Kiafya kila mtu anatakiwa ale matunda ya aina tano kwa siku ili kupata faida zote mwilini.
Matunda humeng’enywa kwa vimeng’enyo tofauti na vyakula mama kama wanga na protini.
Faida kuu za matunda ni kuzuia maradhi, kurutubisha, kinga ya mwili, sukari, nguvu na mafuta asilia.
Faida nyingine ni madini na vitamini mbalimbali yanayosaidia kujenga, kukarabati na hata kuzuia bakteria na maadui wakubwa wakubwa wa miili.

 http://www.risingkashmir.com/wp-content/uploads/2014/06/cherry_fruit-wallpaper-2048x1152.jpg
Cherry
Tunda la ‘Cherry’ hupendwa sana na ndege na lina faida nyingi ambazo husaidia kupambana na maradhi yanayosakama damu au mzungunguko wa maji mwilini kama Jongo.
Jongo ni ugonjwa unatokana na kurithi, kunywa sana pombe, ulaji wa nyama nyekundu, mayai, kutofanya mazoezi.
Ni muhimu kuzingatia kwamba matunda yanatakiwa kuliwa yakiwa katika kitengo kimoja yaani chachu, asidi au alkali.

 
Matunda yenye chachu ni embe, nanasi, chungwa, zabibu na kiwi na kwa upande wa matunda yenye alkali ni tikiti maji, ndizi mbivu, tufaha, pera na strawberry.
Faida za matunda haya ni kinga ya magonjwa. Husaidia kukinga na kupambana na takataka zinazotolewa na mwili au zinazotoka katika mazingira machafu.

 http://jianiteo.com/wp-content/uploads/2012/11/Vitamin-C.jpg
Vitamin C ni muhimu sana mwilini kwani ukosefu wake husababisha uchovu, kukosa usingizi, uvivu, kutokuwa na hamu ya kula.
Ukila matunda yenye vitamin C unapata kinga ya majeraha mwilini, vidonda hupona haraka, huboresha wajihi, haiba na nafsi ya ngozi, mifupa, meno na mzunguko mzima wa damu mwilini, hivyo kusaidia usingizi na kwa watoto kusaidia kukua vizuri.

http://www.specialtyproduce.com/ProdPics/947.jpg

Papai linasaidia kuukinga mwili na kulainisha tumbo ndiyo maana kama mtu amevimbiwa au haendi haja kubwa sawasawa, akila papai humsaidia.

Faida za matunda mwikini

TOFAUTI na vyakula vingine, ndizi zinafaida kubwa sana katika mwili wa binadamu. Kwa mujibu wa wataalamu wa lishe, ndizi zina virutubisho vya aina mbalimbali kama vile, protini, mafuta, kalishiamu, wanga, fosiforas, madini ya chuma, vitamin A,B,C na maji.

Ndizi zina faida zipi katika urembo? Chanzo cha nishati Ndizi zina uwezo wa kumeng’enywa kwa urahisi zaidi, tena zina nishati kubwa, sukari iliyomo katika ndizi ni chanzo kizuri sana cha nishati.

Hivyo naweza kusema kuwa ndizi ikiliwa ipasavyo itakusaidia kujenga mwili na misuli yako kwa ujumla. Husaidia kuondoa chunusi Chunusi ni miongoni mwa matatizo ambayo huwasumbua warembo wengi hususan wanawake.

Je, unafahamu kuwa ndizi mbivu zinaweza kukuondolea tatizo hilo? Kwa kuchanganya ndizi mbivu na maziwa na asali na kisha kuzisaga ili kupata urojo ambao utatumia kupaka kwenye maeneo yaliyoathirika, unaweza kuondokana kabisa na tatizo hilo.

Fanya hivyo kila siku na hakikisha unakaa na mchanganyiko huo kwa muda usiopungua dakika 30 hadi 40, kisha osha na maji ya baridi ikiwezekana yaliyopozwa na jokofu.

Ndizi katika ‘diet’ Ndizi zina nafasi kubwa sana kati kuongeza au kupunguza uzito, hivyo unaweza kutumia ikiwa unahitaji kupunguza ama kuongeza uzito wako.

Kwa wajawazito Ndizi ni chakula kizuri kwa wanawake wajawazito, kwani kina kiwango kikubwa cha ‘folic acid’ ambayo inaweza kufyonzwa kwa urahisi sana na kiumbe kilicho tumboni. Ikiwa mama mjamzito atatumia ndizi mara kwa mara ni wazi kuwa atakuwa mwenye muonekano mzuri na wa kuvutia.
- See more at: http://www.dunialeo.com/sw/posts/browse/health/faida-za-matunda-mwikini#sthash.trZjPdTO.dpuf

No comments

Powered by Blogger.