CHADEMA WAPATA VIONGOZI WAPYA MKOANI SHINYANGA

Hatimaye
Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA),mkoani Shinyanga kimepata
viongozi wapya wa mkoa ,ikiwa imepita miaka mitatu bila ya kuwa na
mwenyekiti wa mkoa wa Chama hicho.
Awali mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Shinyanga alikuwa Philip Shelembi Magadula,aliyefariki dunia mwaka 2011.
Akisimamia
uchaguzi kupata viongozi wapya juzi mbunge wa jimbo la Maswa Mashariki
mkoani Simiyu (CHADEMA),Sylivester Kasulumbayi(PICHANI), uliofanyika
mjini Shinyanga, alisema lengo la uchaguzi ni kuendelea kuimarisha
chama na kujipanga katika chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2015.
Kasulumbayi aliwataja viongozi hao wapya waliochaguliwa kuwa ni Peter
Frank,Mwenyekiti wa Chadema mkoa, katibu ni Zacharia Thomas, Mwenyekiti
wa Baraza la Vijana (Bavicha), Chripin Simon, Katibu BAVICHA ni Ezekiel
Joseph.
Kwa upande wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA),mwenyekiti ni Rachel Mashishanga, ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum (CHADEMA),jimbo la Shinyanga Mjini huku katibu wake akiwa ni Winfrida Daudi.
Alimtaja mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoa wa Shinyanga aliyechaguliwa kuwa ni Mhidini Ibrahim.
Kufuatia
uchaguzi huo ambao ulifanyika kwa amani ,Kasulumbai aliwataka viongozi
hao wapya (CHADEMA),mkoa kufanya kazi kwa ushirikiano bila ya kuwa na
makundi ikiwemo kuzingatia sera na katiba ya Chama.
source: Malunde1 blog -Shinyanga
Post a Comment